Kwa mara ya pili Khadija Kopa akiri kutofahamu Mahusiano kati ya binti Zuchu na Diamond

Mahusiano ya Zuchu na Diamond wanayajua wao ,sijafahamishwa - Khadija Kopa alisema.

Muhtasari

• "Siwezi kushawishiwa na kwa vyovyote mimi nina heshima  Zangu kulingana na mila zetu mshichana anapopata mume lazima wazazi wajulishe kwa pande mbili zote," Kopa.

Diamond Platnumz,zuchu na Khadija Kopa
Diamond Platnumz,zuchu na Khadija Kopa

Khadija Kopa mwimbaji wa muziki wa Taarab na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania ambaye pia ni mamake mzazi msanii maarufu wa Bongo Zuchu kwa mara ya pili amezungumzia kutoyafahamu mahusiano ya ndoa kati Bintiye Zuchu na  Nyota wa Bongo Diamond Platnumz

Kulingana na Khadija Kopa Bintiye Zuchu hajawai kumfahamisha wala kumtambulisha kwa Diamond akisimulia kuwa mapenzi yao wanayajua wao wenyewe.

"Siyajui kamwe mahusiano ya Binti yangu Zuchu na msanii Diamond nadhani ni siri yao na Muumba wao kwani sijawahi fahamishwa, kwa vyovote vile ikiwa ni mahusiano ya kweli waje nyumbani wajitabulishe kulingana na mila zetu,"alisema Khadija Kopa.

 

Mtunzi huyo wa Taarab alikiri hayo Kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao akisema kuwa yeye ni mzazi ambaye upendezwa na utaratibu wa kufanya mambo hadharani, huku akitaja ikiwa Mwanawe yuko kwa Mahusiano ni lazima afuate mila na desturi kwani hawezi kamwe kukumbali ndoa ambayo hajafahamishwa.

"Siwezi kushawishiwa na kwa vyovyote mimi nina heshima  Zangu kulingana na mila zetu mshichana anapopata mume lazima wazazi wajulishe kwa pande mbili zote ndiposa swala la kulipiwa mahari itekelezwe kwa wakati unaofaa kwa hivo Diamond na binti yangu Zuchu hawajaona ",alisema Kadhija Kopa.

Hiyo ni mara ya pili kwa Khadija Kopa kukiri kuwa hayajui mahusiano kati ya bintiye Zuchu na  msanii Diamond.