"Ukomavu" Alikiba ajibu Harmonize akimpigia saluti kama mfalme wa Bongo Fleva

Harmonize alisema hivi karibuni anafikisha miaka 30 na pia mwanawe anafikisha miaka 5 na kumtaja binti huyo kama kielelezo ambacho kimempa msukumo wa kujioa kama amekua sasa.

Muhtasari

• “Hivi karibuni nafikisha miaka 30, kwa hiyo nakua. Halafu kingine mimi nina mtoto wa kike, anafikisha miaka 5 hivi karibuni, na anapokuwa ananihimiza." Harmonize alisema.

Siku chache baada ya Harmonize kumpa Alikiba maua yake na kumtaja kama mfalme wa muziki wa Bongo Fleva, msanii huyo wa Kings Music amemjibu kwa kumpa hongera na kutaka tamko lake hilo kama la kikomavu.

Harmonize katika mahojiano yake na vyombo vya habari baada ya kutua nchini Tanzania na tuzo tatu za AEUSA 2023 kutoka Marekani, alisema kwamab hana ubaya na mtu yeyote, akimtaja binti yake ambaye anaelekea miaka 5 sasa kama kielelezo kikuu cha kutaka kukaa sawa na kila mtu.

Papo hapo alizungumzia ile klipu ya siku fulani nyuma alipokwenda kwenye Alikiba alikuwa anafanya mahojiano na kumrukia mabegani kwa mbwembwe na alizungumzia tukio hilo akisema kwamba alikuwa anataka kuonesha ulimwengu kwamba hana tatizo hata kidogo na Alikiba.

“Kwenye jamii kuna mentality kuwa mimi nina shida na @OfficialKiba lakini mimi sikufichi na nakwambia ukweli kabisa, Alikiba ni kati ya watu ambao mimi nimejifunza muziki kutoka kwao, hatujawahi kukutana kwenye tatizo lolote na hatujawahi hata kushare wanawake. Namheshimu ana mchango mkubwa sana katika hii sana huwezi kupinga hilo, sisi tumejifunza kupitia yeye, tumekua tunamkuta Ali anafanya vitu vingi vikubwa tunapata ile mentality kwamba kumbe inawezekana kufanya huu muziki kukupa heshima na kulipa heshima taifa lako,”

“Hivi karibuni nafikisha miaka 30, kwa hiyo nakua. Halafu kingine mimi nina mtoto wa kike, anafikisha miaka 5 hivi karibuni, na anapokuwa ananihimiza. Sitaki mwanangu akue akute sijui baba ana matatizo na mtu huyu, nitamweka mwanangu kwenye mazinginra ya kujiuliza kwa nini baba hapendani au kupatana na huyu, kwa hiyo ninakua,” aliongeza.

Alikiba kupitia ukurasa wake wa X alirepost klipu hiyo ya Harmonize akizungumza na kuweka emoji ya makofi huku akiambatanisha na neno moja tu, “ukomavu.”