Bilionea wa Youtube 'Mr Beast' azikwa siku saba na kufukuliwa kwa lengo la umaarufu

Hii ni mara ya pili kwa muunda maudhui huyo kuzikwa na kufukuliwa

Muhtasari

•Mr Beast kwenye video yake kama tu jinsi wafu uzikwa na nguo nyeusi alifuata mtindo huo huo huku jeneza lake likipabwa kwa kioo sehemu ya juu kioo kilichomuonesha akiwa ndani ya kaburi lake la siku saba

Mr Beast
Mr Beast
Image: Screengrab

Mtengeneza maudhui maarufu duniani kwenye ulimwengu wa Youtube almaarufu Mr Beast wiki hii amekuwa gumzo mitaa baada ya kufanya maajabu ya kuzikwa na kufukuliwa baada ya siku saba.

Mwanablogu huyo ambaye ndiye mtengeneza maudhui tajiri zaidi duniani kwenye jukwaa la Youtube inasemekana kuwa alizikwa hai na video za moja kwa moja kurekodiwa kwenye mtandao wake.

Mtengeneza maudhui huyo inasemekana kuwa lengo lake ilikuwa kupata zaidi ya wafuasi billioni mia mbili kwenye mtandao wake wa Youtube ikitajwa kuwa ni mmoja wa waunda madhui ambao upokea kiasi cha hela cha juu kupitia kurasa zao.

Mr Beast kwenye video yake kama tu jinsi ambavyo  wafu uzikwa na nguo nyeusi alifuata mtindo huo huo huku jeneza lake likipabwa kwa kioo sehemu ya juu kioo kilichomuonesha akiwa ndani ya kaburi lake la siku saba.

Ndani ya jeneza hilo alilokuwa amezikwa kwa Siku saba kulikuwemo na maua,taa,vyakula na hata vinywaji huku marafiki zake wakicheza na kuimba huku wakimsubiri atoke nchini ya ardhi alopozikwa.

Licha ya kuzikwa na kulala kwa jeneza kwa siku saba mtengeneza maudhui huyo alitoka ndani akiwa mzima ,hii ni mara ya pili kwa muunda maudhui huyo kuzikwa hai na kufukuliwa ili kujitafutia umaarufu.