‘Watoto hawakuongezi thamani yeyote’ – Andrew Kibe awashauri wanaume

Alisistiza kuwa wakati pekee ambapo mtu anaitajika kupata watoto ni pale anapoona kuwa amefaulu maishani,vinginevyo watoto pia huenda wakafeli kama mzazi wao.

Muhtasari

• Kulingana na yeye, watoto hawaongezi thamani yoyote kwao ila huja tu kutumia rasilimali walizotafuta kwa jasho.

• “Bro usiwe na watoto kwa sababu watoto hawakuongezei thamani yeyote kama mwanaume,”

Andrew Kibe
Andrew Kibe
Image: Screengrab

Mwanablogu na muundaji maudhui wa Marekani Andrew Kibe amewashauri  wanaume wasipate  watoto.

Kulingana na yeye, watoto hawaongezi thamani yoyote kwao ila huja tu kutumia rasilimali walizotafuta kwa jasho.

“Bro usiwe na watoto kwa sababu watoto hawakuongezei thamani yeyote kama mwanaume,”alisema.

“Watoto huja tu kuchukua rasilimali zozote unazotafuta,”Kibe aliongeza.

Alisistiza kuwa wakati pekee ambapo mtu anahitajika kupata watoto ni pale anapoona kuwa amefaulu maishani,vinginevyo watoto pia huenda wakafeli kama mzazi wao.

"Wakati pekee ambao unatakiwa kupata watoto ni wakati umeshinda kisha sasa unaweza kuleta wazo la kupata watotokwa sababu watoto hawawezi wakafaulu ikiwa wewe mwenyewe umeshindwa.

Hata hivyo Kibe aliwashauri wale ambao wamekisha kupata watoto wachukue jukumu la kuwalea vyema kwa kuiwapa maitaji yao yote.

“lakini ikiwa una watoto, watunze vizuri,” Kibe alishauri.

Matamshi ya Kibe yanatoa kisengere nyuma kwa matamshi ya askofu Jackson Ole Sapit ambaye alishauri kuwa,serikali inapaswa kuweka sheria ya kuruhusu watu kupata watoto wasiozidi wanne.

Kasisi huyo alitofautiana na baadhi ya viongozi wa kisiasa waliowashauri Wakenya kupata watoto wengi.

Alisisitiza umuhimu wa kupanga uzazi ili kupunguza shinikizo kwa uchumi na kuongeza idadi ya Wakenya wanaolipa zaka na ushuru. 

“Ni vyema tuanzishe kampeni ya kuwaambia Wakenya kupunguza idadi ya watoto hadi 4,” alisema Ole Sapit.

Hata hivyo mwanablogu huyo amepokea ujumbe wa ajabu kutoka kwa mwanamuziki KRG the Don kutokana na vita vyao vya maneno vya hapo awali,akimuonga na kumtishia Kibe.

“Nakukaribisha na nakupa ahadi kuwa nitakuja kukulaki kwenye uwanja wa ndege lakini nakuambia kuwa lazima nitakufinya,” Krg aliisema.

Kibe ambaye anapanga hafla ya kurudi nchini alimjibu KRg akisema kuwa liwe liwalo lazima mipango yak itimike na wala hatishwi na lolote.