Kwa nini tulifunga chaneli ya Youtube ya Andrew Kibe - Google

Fahamu kilicho fanya chaneli za Andrew Kibe kufungwa mbali na kuwa na wafuasi wengi

Muhtasari

Kibe kwa muda amekuwa akiarifu kundi la mashabiki wake kwamba mara tu atakapomaliza kutumia YouTube, atapakia maudhui yake kwenye jukwaa lingine.

Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Muunda maudhui wa Marekani, Andrew Kibe.
Image: INSTAGRAM

Mkuu wa Mawasiliano katika Google Africa Dorothy Ooko ameeleza ni kwa nini chaneli za YouTube za Andrew Kibe zilifungwa.

Ooko alisema Kibe alikwenda kinyume na kanuni na masharti ya YouTube na alizuiwa kutumia vipengele vya jukwaa.

Alieleza kuwa baada ya chaneli moja kuwekewa vikwazo, Kibe aliendelea kutumia akaunti tofauti ili kuepuka vikwazo.

"Alitumia chaneli nyingine kuzunguka vizuizi hivi kama kukwepa, na kusababisha kusitishwa kwa chaneli zake zote," Ooko alisema kwenye chapisho la X.

Ooko alikuwa akimjibu shabiki wa Kibe Marian Wairimu ambaye alikuwa anataka kujua sababu YouTube kwa kusitisha chaneli ya Kibe.

"Utamaduni wa kughairi hauruhusiwi kukita mizizi katika uundaji wa maudhui. Kusitishwa kwa Andrew Kibe kwa akaunti za YouTube hakuhusu ujumbe wake bali ni shambulio la moja kwa moja kwa wabunifu.

Rejesha akaunti zake.  Mariam alisema. Kwa upande wake, Kibe alisema hajapokea barua pepe inayoonyesha ukiukaji, jambo lililosababisha  akaunti zake za mitandao kufugwa.

Unaweza kunionyesha barua pepe za ukiukaji huo? Hiyo ndiyo utaratibu, sawa? Ninamaanisha kwamba hakuna njia ambayo YouTube inaweza kuzuia kabisa kituo chochote ambacho kina zaidi ya video 3000 bila karatasi?" Aliuliza.

Kibe kwa muda amekuwa akiwajulisha mashabiki wake kwamba mara tu atakapomaliza kutumia YouTube, atapakia maudhui yake kwenye jukwaa lingine. 

Watu maarufu ambao akaunti zao zilikatishwa wakati fulani ni pamoja na Diamond Platnumz, ambaye anaendesha moja ya akaunti kubwa zaidi barani Afrika na zaidi ya watu milioni 7 wanaofuatilia. Akaunti yake ilisitishwa mnamo 2022 lakini alifanikiwa kuirejesha.