Achana na watoto wa kiume Andrew Kibe amwambia Mchungaji Dorcas

Kibe alisema wanaume wana nafasi bora kuwashauri wavulana, mama hafai kuzungumza na watoto wa wavulana wa umri fulani.

Muhtasari

•Katika video kwenye mtandao wake wa kijamii, Kibe alisema Mchungaji Dorcas anapaswa kutumia nguvu kuzungumza na wanawake.

•Alisema wanaume wana nafasi nzuri ya kuwashauri wavulana akisema kuwa mama hatakiwi kuruhusiwa kuzungumza na watoto  wa kiume zaidi ya umri fulani.
 

Kibe na Dorcas.
Kibe na Dorcas.
Image: Maktaba

Mwanablogu Andrew Kibe amemtaka Mke wa Naibu wa Rais Mchungaji Dorcas Rigathi kuachana na masuala ya watoto wa kiume na badala yake ajikite katika kuwapa ushauri washichana nchini ushauri.

Katika video kwenye mtandao wake wa kijamii, Kibe alisema Mchungaji Dorcas anapaswa kutumia nguvu kuzungumza na wanawake.

Alisema wanaume wana nafasi nzuri ya kuwashauri wavulana akisema kuwa mama hatakiwi kuruhusiwa kuzungumza na watoto wa wavulana wa umri fulani.

“Mke wa naibu wa rais  asiruhusiwe kuzungumza na wavulana  waliovuka umri fulani kwa sababu unataka kuwachukulia kama watoto na hapo ndipo wengi wanapofanya makosa... Mtawaangamiza hawa wavulana, kabla hamjajua watakuwa vijana wavivu," alisema.

Kibe alisema mke wa naibu rais anapaswa kutembelea shule za wasichana na kuwafundisha wanawake jinsi ya kuwa kama yeye badala ya kuhangaika na wavulana.

Mwanablogi huyu wa youtube  alisema kwamba mke wa naibu rais anapaswa kusaidia kuunda mifumo bora ambayo inalinda familia.

"Nenda shule, ongea na wasichana na wafundishe jinsi ya kuwa wake na mama''.

"Wafundishe jinsi ya kufanikiwa kama nyinyi.  Unaweza kushughulikia hilo halafu tutawashughulikia wanaume. " alisema Kibe. Alisema mpango wa kuwasaidia wanaume hauwezi kutoka kwa wanawake.