Awinja asema atakayemuoa lazima awe na hekari 50 za ardhi

Mchekeshaji huyo sasa anajiunga na orodha ya mastaa wa kike wa Kenya ambao wametangaza bei ya mahari yao hadharani.

Muhtasari

• Mcheshi huyo alitaja hitaji lake la bei ghali kama jambo la msingi akieleza kuwa hiyo ndiyo ndoto ya maisha yake.

• ”Ule atanioa niseme mapema mimi haya ndio maisha ninayotaka. Staki vitu mingi,hekari 50  za ardhi tu”

Jacky Vike
Jacky Vike
Image: INSTAGRAM

Mwigizaji na muunda maudhui Jacky Vike  maarufu kama Awinja,ametangaza wazi anachohitaji kutoka  mwanaume yeyote ambaye angetaka kumuoa.

Awinja alitumia akaunti yake ya Instagram iliyofuatwa kwa kiasi kikubwa  na kusema kuwa ikiwa kuna mwanaume yeyote ambaye ana matamanio ya kumuoa lazima awe na ekari 50 za ardhi.

Alichapisha video yake akiwa kijijini, akilisha ng'ombe na mbuzi, akitembea katika shamba la mahindi huku akieleza  nia yake ya kuishi maisha ya mashambani wakati atakapoolewa.

Mcheshi huyo alitaja hitaji lake la bei ghali kama jambo la msingi akieleza kuwa hiyo ndiyo ndoto ya maisha yake.

”Ule atanioa niseme mapema mimi haya ndio maisha ninayotaka. Staki vitu mingi,hekari 50  za ardhi tu” alinukuu.

Wanamtandao na mashabiki  walitoa maoni yao  kuhusu sheria na masharti ya mcheshi huyo.

Wengine walimkashifu kwa kuwa na uchu kutaka mali wakisema kwamba hakuna kitu cha msingi kuhusu ekari 50 alizotaka huku wengine wakijitolea kutoa zaidi ya hekari 50 za ardhi ili kuwa wenye bahati ya kumuoa Awinja.

"Wanawake wanapaswa kuamka na kufanya kazi ... na wanaume dhaifu wanafanya maisha kuwa magumu ikiwa unataka kitu fulani tafuta pesa ununue... uyu anapewa ekari 50 aje sasa, nunua,”alisema mwanamtandao mmoja.

”Ako sawa kabisa, huyu sasa ndio anabamba..unaona Waluhya wanaitisha vitu vya maana,"aliongeza shabiki mwingine.

”Hiyo shamba yote inatoka wapi..hiyo ni takriban trilioni ..je wewe unatosha trilioni?” mwanamtandao mwingine aliuliza.

Mchekeshaji huyo sasa anajiunga na orodha ya mastaa wa kike wa Kenya ambao wametangaza bei ya mahari yao hadharani.

Tangazo lake lilijiri siku chache baada ya sosholaiti Mkenya anayejulikana kama Mylee Stacy kusema kuwa mahari yake ilikuwa ya thamani ya bilioni 800.

Mpenzi wa Eve Mungai alianzisha mchakato huo baada ya kusema kwamba atatoa Milioni 10 kama mahari kwa mwanablogu huyo mahiri.