Muigizaji Awinja afunguka baada kuji'surprise na gari la kifahari

kununua gari ni mojawapo ya shukrani kwangu kwa kazi nzuri ninayofanya Awinja asema

Muhtasari

• Awinja alinunua gari la kifahari aina ya Jeep siku chache zilizopita akisema kuwa imekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Muigizaji Awinja
Muigizaji Awinja

Muigizaji Jacky Vike almaarufu Awinja Nyamwalo amefunguka siku chache baada ya kununulia gari  aina ya 'Jeep Wrangler'  gari ambalo amesema amelitamani kwa muda mrefu.

Awinja alisema kuwa amewekeza kwa muda mrefu kununua gari hilo ili kutimiza ndoto yake kwani baadhi ya malengo yake ni kujirudishia shukrani  kwa bidii zake kuigiza.

"kufanikisha malengo yangu ya kujinunulia gari hilo la kifahari nimeweza kuekeza kwa muda mrefu ili kutimiza ndoto yangu, gari hilo aina ya Jeep limekuwa tamanio langu kwa magari yote kwa kuwa nilipata ufahamu wa kulijua zaidi kupitia marafiki wangu.

Kulingana na Awinja yeye hufanya kazi zake za uigizaji akiwa na matumaini kuwa kazi anazozifanya zitamletea mafanikio kwa maisha yake ili kujikimu kimaisha na pia kujirudishia shukrani kwa kujinunulia chochote ambacho ni tamanio la roho yake.

"Kuigiza ni jambo gumu zaidi ila mimi hujisatiti kuakikisha chochote naigiza kinaweza kuwa manufaa kwa maisha yangu,ndio maana najituma sana ili niweze kutimiza ndoto zangu na kujirudishia shukrani kwa vyovyote vile, kununua gari ilikuwa mojawapo ya shukrani kwangu kwa kazi nzuri.

 

 

 

 

Mchekeshaji Awinja
Mchekeshaji Awinja