Christina Shusho kufanya tamasha kubwa Kenya mwishoni mwa mwaka huu

Aidha alisema kuwa timu yake ilikuwa ikishirikiana na Mwalimu Churchill (Daniel Ndambuki) kwa ajili ya kuandaa tamasha hilo.

Muhtasari

• Kupitia akaunti yake ya X, mwimbaji huyo alisema ameamua kuwa na tamasha kwa ajili ya mashabiki wake wa Kenya kutokana na mahitaji kuongezeka.

• "Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya tamasha nchini Kenya, timu yangu na mimi tunafanya kazi na Mwalimu Churchill kuwa na tamasha mnamo Desemba 31, 2023."

Christina Shusho
Christina Shusho
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Christina Shusho sasa amewahakikishia mashabiki wake kuwa atafanya tamasha nchini Kenya.

Kupitia akaunti yake ya X, mwimbaji huyo alisema ameamua kuwa na tamasha kwa ajili ya mashabiki wake wa Kenya kutokana na mahitaji kuongezeka.

Aidha alisema kuwa timu yake ilikuwa ikishirikiana na Mwalimu Daniel Ndambuki kwa ajili ya kuandaa tamasha hilo.

"Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya tamasha nchini Kenya, timu yangu na mimi tunafanya kazi na Daniel Ndambuki kwa tamasha mnamo Desemba 31, 2023..)," mwimbaji huyo alisema.

"Kutokana na maombi ya wengi, nyinyi ni watu wangu muhimu. Tarajia tamasha la usiku mmoja tarehe 31 Desemba. Churchill anashughulikia hili. Tuonane hivi karibuni 254," alisema.

Mashabiki wa muziki wamezua gumzo kuhusu nyimbo zake za kuabudu kwenye X.

Mashabiki wengine wamekuwa wakidai msanii huyo  wa injili hana uhalisi katika mashairi ya nyimbo zake kwani yeye anazipata kutoka kwa bibilia.

Hata hivyo, wengi walivutiwa na jinsi anavyojumuisha maandiko katika nyimbo zake, ikilinganishwa na wanamuziki wengine wa injili.

Christina Shusho alijibu Wakenya mtandaoni wakijadili nyimbo zake za injili.

@kimrobstan...nashangaa nyie mnashangaa. Hivi ndivyo muziki wa injili unavyotakiwa kuwa. Imba kutoka katika maandiko. (Biblia)

@SpaxGenius...Shida ni hamjui bibilia kwa hiyo inaonekana ni ya ajabu kwenu nyote

@fanconsul.., nyie mnachekesha. Nyimbo nyingi za injili zimechukuliwa kutoka katika Biblia neno kwa neno. Umekuwa ukiishi wapi?

@MwawanaMuema...Alifanya vivyo hivyo na "Bwana Umenichunguza". Moja kwa moja kutoka Zaburi 139

@mkoloni_...Tunahitaji tamasha Kenya tunalilia mioyo yetu

@azdaknick......"Utukumbuke eeh" ,napenda nyimbo zake zinanibariki sana.”

Mashabiki hao waliendelea kutoa maoni yao huku wakimsifu mwimbaji huyo kwa nyimbo zake ambazo wamesema zinafariji mioyo yao na kuwaleta karibu na Mungu.

"Nataka kufikisha shukurani za dhati kwa wakereketwa wote wa Christina Shusho kwa kufanya chaguo sahihi. Sio tu ameshinda mioyo yetu bali pia roho zetu.”

Christina Shusho anafahamika kwa nyimbo zake maarufu kama vile: Unikumbuke, Mtetezi wangu, Agano, Nipe Macho na nyinginezo