Prince William hana mpango wa kuonana tena na Harry, 'labda kwenye mazishi ya familia!"

“Ni vigumu sana kuona tukio lingine lolote, isipokuwa labda mazishi ya familia, ambapo akina ndugu wangekuwa mahali pamoja,” akasema Hewson.

Muhtasari

• Wawili hao hawajakuwa na uhusiano mwema wa kindugu tangu Harry alipotoa kitabu chake cha kusimulia jinsi kakake nkubwa pamoja na familia yote ya kifalme iko kinyume na ndoa yake kwa Markle.

Prince Harry asema nduguye Prince William alimpiga 2019
Prince Harry asema nduguye Prince William alimpiga 2019
Image: US Weekly

Mgawanyiko mkubwa unazidi kushuhudiwa kati ya Prince Harry na kakake mkubwa Prince William ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Harry kuachia kitabu chake ambamo alielezea jinsi kakake mkubwa kwa wakati mmoja alimpiga kisa tu kuoana na Meghan Markle.

Taarifa mpya kutoka kwa mtaalamu wa masuala yanayoendelea katika kasri la Birmingham, Sarah Hewson, anadai kwamba William hana mpango wa kumsamehe wala kuonana tena na kakake mdogo, Prince Harry – isipokuwa tu nyakati za kubidi kama msiba wa kifamilia.

"Tumeona tu Harry akirudi kwa hafla kubwa za kifamilia - alikuja na Meghan kwa sherehe za Platinum Jubilee, alirudi kwa mazishi ya Prince Philip, kisha kwa mazishi ya bibi yake Malkia Elizabeth II. Na kisha bila shaka kwa kutawazwa kwa baba yake, ambayo ingawa ilikuwa ziara ya muda mfupi sana, "Hewson alimwambia Fabulous, kupitia Sun.

"Lakini hatuna hafla yoyote kubwa ya familia au serikali karibu," aliendelea. "Siwezi kufikiria ndoa yoyote ya kifalme ijayo, ubatizo, kwenye shajara ambayo ingemrudisha Harry."

Hewson alisisitiza kwamba hata Harry, 39, au mkewe Meghan Markle, 42, watahudhuria mkutano wa familia ya kifalme huko Sandringham wakati wa Krismasi, akiongelea kwamba kuonekana kwa wawili hao itakuwa "mbaya sana."

“Ni vigumu sana kuona tukio lingine lolote, isipokuwa labda mazishi ya familia, ambapo akina ndugu wangekuwa mahali pamoja,” akasema Hewson.