Baraka The Prince aeleza chanzo cha chuki baina yake na Alikiba

Baraka alitoka stundio baada ya kutajwa kwa jina Alikiba

Muhtasari

•Diamond kunitakia heri njema katika siku yangu ya kuzaliwa ndio sababu iliyomfanya Alikiba kunigombanisha.

Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Baraka the Prince, Alikiba Msanii Baraka amemkana Alikiba,
Image: Instagram

Siku moja baada ya Msanii Baraka The Prince kukasirika na  kutoka katikati ya mahojiano kwenye kituo kimoja cha radio baada ya kutajiwa jina la Alikiba amejitokeza na kusimulia uhasama kati yake na staa huyo  wa Bongo

Msanii huyo ambaye amekuwa na chuki na Alikiba kwa muda mrefu alifanyiwa mahojiano na wanablogu wa mitandao huku akisema kuwa Alikiba alimkashifu baada ya picha aliyoweka kwenye mtandao wake huku msanii Diamond akimpongeza kwa hatua hiyo.

"Ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa wakati nilipoenda kwa mtandao wangu kuposti picha yangu watu wengi walinishabikia ila wakati Diamond alipotuma ujumbe wake akinishabikia kwa siku yangu jambo hilo lilimkera Alikiba,"alisema.

Baraka the Prince kwenye mahojiano hayo alieleza zaidi kuwa baada ya kumshukuru Diamond kwa kumshabikia siku yake ya kuzaliwa msanii Alikiba alimpigia simu huku akimrushia maneno makali kwa sababu ya maogezi yake na Diamond

"Nilikuwa nasafiri na gari langu nilipokea siku kutoka kwa Alikiba akinigombanisha kwa nini niliweza kujibu ujumbe wa Msanii Diamond jambo hilo lilinikera mno nikishidwa ni vipi msanii Diamond kunitakia heri njema kwa siku yangu ya kuzaliwa ilikuwa tisho kwa Alikiba.

 Baraka the Prince alionesha jinsi chuki ilivyokithiri baina yake na bosi wake wa lebo ya zamani, Alikiba baada ya kuzua na kutoka katika kituo kimoja cha redio kwa jina Mjini FM nchini Tanzania, baada ya kuondoka kwa fujo studioni mtangazaji alimpotajia jina Alikiba akilenga kumuuliza swali kuhusu rafiki wake wa zamani kwenye lebo ya Kings Music.