Georgina Njenga azungumza kwa mara ya kwanza kuhusu picha zake

Mtayarishaji wa maudhui pia alimsifu aliyekuwa mume wake, Tyler Mbaya akifichua kuwa ndiye aliyemwangazia habari hizo.

Muhtasari

• Alifichua kuwa alijua kuhusu swala hilo miaka 3 kabla ya kutishwa na kukashifiwa na mtu huyo aliyekuwa na picha zake.

Georgina Njenga
Georgina Njenga
Image: INSTAGRAM

Aliyekuwa mpenzi   wa Tyler Mbaya (Baha)  Georgina Njenga, amezungumza kuhusu picha za utupu zilizodaiwa kuwa zake kwa mara ya kwanza tangu zilipovuma.

Shabiki mmoja alimuuliza mama huyo wa mtoto mmoja jinsi alivyoweza kukabili hali hiyo ngumu na hatua zilizochukuliwa dhidi ya mhusika aliyeeneza picha hizo.

Georgina alisema kuwa hatamtaja mtu huyo kwa jina kwa sababu labda hiyo ndiyo ilikuwa nia yao, kumfanya ashindwe kuimarika na kumshinikiza kusema maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Alifichua kuwa alijua kuhusu swala hilo miaka 3 kabla ya kutishwa na kukashifiwa na mtu huyo aliyekuwa na picha zake.

"Sidhani kama niko mahali pazuri kusema ni nani kwani labda ndicho alitaka niende na kusema ni mtu huyu, nilijua kwa miaka mitatu. Alianza kunitisha mnamo 2020 tulipofichua tu uhusiano wetu na Tyler Ata haikumaliza siku mbili.” Alieleza.

Georgina pia alimsifu aliyekuwa mume wake, Tyler Mbaya akifichua kuwa ndiye aliyemwambia habari hizo.

”Aliyegundua kwanza ni yeye,aliniambia twende rooftop alikokuwa amekaa,nikashtuka. Kwangu nilidhani ni kifo. Alinikalisha chini na kuniambia kwamba angesimama na mimi. Wakati huo, nyanyangu alikuwa hospitalini hivyo kwangu nilifikiri kuwa ni kifo,” Njenga alisema.

Alieleza kuwa Baha alimhakikishia mapenzi na kumuunga mkono na pamoja na upendo kutoka kwa familia na marafiki hasa mama yake mzazi ilikuwa rahisi kwake kukabiliana na tatizo hilo.

”Nilikingwa kutokana na yale ambayo watu wengine walikuwa wanasema kabisa kwa sababu mama yangu aliniunga mkono. Hakujua kuhusu hilo lakini nilimpigia simu na kumwambia. Kwa sababu Baha alisimama na mimi,pamoja na marafi zangu wa karibu nafikiri hilo lilinipa moyo,”alisema.