‘Nahitaji maombi yenu’ Nasra Yusuff akiri anakumbwa na msongo wa mawazo

Nasra alisema anapitia hali ngumu ya msongo wa mawazo ambayo inamfanya awe na hisia za kujitoa uhai.

Muhtasari

• Kupitia ukurasa wake wa Insta story, Nasra alisema kwamba kwa sasa anapitia hali ngumu ya msongo wa mawazo ambayo inamfanya awe na hisia za kujitoa uhai.

• “Nyote mnamdhihaki Azziad kwa kutaka kujitoa uai,wakati mimi niko katika hali hiyo hivi sasa,”

Nasra Yusuff
Nasra Yusuff
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji na mwimbaji wa nyimbo za Oromo Nasra  Yusuff amejitokeza na kusema wazi kuwa anapitia hali ngumu ya msongo wa mawazo.

Kupitia ukurasa wake wa Insta story, Nasra alisema kwamba kwa sasa anapitia hali ngumu ya msongo wa mawazo hali inayomfanya ahisi kujitoa uhai.

“Nyote mnamdhihaki Azziad kwa kutaka kujitoa uhai, 3wakati mimi niko katika hali hiyo hivi sasa,”ulisoma sehemu ya ujumbe wake wa Insta story.

Kama njia moja ya kuonyesha kulemewa na mawazo, Nasra aliwaomba mashabiki wake wasimlaumu kwa lolote analowazia kulifanya kuhusiana na maisha yake.

“Nikifanya hivyo, tafadhali msinifanyie mzaha, nilijaribu,”aliandika.

Ujumbe huo mzito uliambatana na ujumbe ambao ulisimulia hisia nzito za mcheshi huyu ambaye kwa hakika ameonyesha wazi hali ya msongo wa mawazo.

“Nimechoka kudanganya na kujifanya kuwa niko sawa,siko sawa,nahitaji msaada, nahitaji maombi, nahisi napoteza. Mimi nipo kila mara kwa ulimwengu wote na sasa ninahitaji tu kutendewa hivyo,iwe kutoka kwa mtu ninayemjua,au mtu yeyote Yule,”alichapisha.

Image: screengrab

Visa vya watu mashuhuri kukumbwa na msongo wa mawazo vinazidi kushuhudiwa, licha ya wengi wao kususia kujitokeza hadharani kusimulia hali hiyo.

Kisa cha Nasra kimejiri siku chache tu baada ya Muunda maudhui wa Kenya Azziad Nasenya kujitokeza na kusimulia hali sawia ya msongo wa mawazo.

Nasenya alieleza kuwa alighadhabishwa baada ya mashabiki kumkashifu baada ya kushiriki katika wimbo wa Mejja na Femi One ‘Utawezana’ ambao ulivuma kweli.

Kulingana na mashabiki Azziad alidensi visivyositahili katika wimbo huo, na hivyo kumkosoa vikali,j ambo ambalo lilimsababishia msongo wa mawazo hadi kuwazia kujitoa uai.