Zari ashangazwa na swag ya Diamond kuvaa suruali zinazompwerepweta siku hizi

Mtindo wa Diamond katika siku za hivi karibuni umekuwa ni wa kuchangua suruali kubwa kubwa zinazoonekana kama zimemvaa yeye., mtindo huo unahusishwa na Asake kutoka Nigeria.

Muhtasari

• Wawili hao waliachana mwaka 2018 baada ya uhusiano wa karibia miaka 5 na kubarikiwa na watoto wawili, binti na mvulana.

Diamond na suruali kubwa
Diamond na suruali kubwa
Image: Instagram

Babymama wa Msanii Diaomond Platnumz, Zari Hassan ameonesha kushangazwa na mtindo wa mavazi ya mwanamuziki huyo katika siku za hivi karibuni.

Zari alikwenda kumkuta Diamond katika gari wakati msanii huyo alikuwa anapita nchini Afrika Kusini anakoishi mama wa watoto wake.

Zari alianza kumuuliza Diamond kuhusu nguo kuashiria kwamba msanii huyo pengine alikuwa anasubiri mavazi yake ambayo alikuwa ameagiza lakini yakachelewa kufika.

Hapo hapi Zari pia alitia neno kuhusu mtindo wa Diamond kuvaa mavazi yanayokaa kumpwerepwetr akituhumiwa kuiga mtindo huo kutoka kwa msanii wa Nigeria, Asake.

“Kwani nguo hazijafika? Sasa si wamenitumia ratiba jana, lakini siku hizi wewe bwana uko na mtindo wako wa kuvaa, unavaa visuruali vikubwa vikubwa,” Zari alisema kabla ya jamaa mmoja kuingilia mazungumzo yao kuwasalimia.

Zari aliweka suala hilo la mavazi pembeni na kuleta suala la familia akimwambia Diamond kwamba watoto walikuwa wanataka kuonana naye.

Hata hovyo, Diamond alikataa kukubali kukutana na wanawe Tiffah na Nillan akiahidi kufanya hivyo siku inayofuata kabla ya kuondoka nchini Afrika Kusini.

Wawili hao waliachana mwaka 2018 baada ya uhusiano wa karibia miaka 5 na kubarikiwa na watoto wawili, binti na mvulana.

Mtindo wa Diamond katika siku za hivi karibuni umekuwa ni wa kuchangua suruali kubwa kubwa zinazoonekana kama zimemvaa yeye.

 Mtindo huo unahusishwa haswa na wasanii wa kizamani haswa wa Rhumba kutokea DRC lakini katika kizazi kipya, unasemekana kuanza kukumbatiwa na chipukizi wa Nigeria, Asake.