Samidoh apagawa na furaha baada ya kukutana na Zari Hassan

“Jioni ya leo, nimejivunia kuwa na fursa nzuri ya kutumbuiza Wanawake katika Biashara Kenya Ilikuwa nzuri kushuhudia wanawake bora wakitunukiwa tuzo kwa ubora wao" Samidoh aliandika.

Muhtasari

• Samidoh alisema kwamba ilikuwa furaha ya kupata nafasi adimu ya kuhudhuria mkutano wa wanawake katika biashara na ujasiriamali.

Zari na Samidoh.
Zari na Samidoh.
Image: Facebook

Mapema Ijumaa Radiojambo.co.ke iliripoti ujio wa mjasiriamali wa Uganda mwenye makaazi yake nchini Afrika Kusini, Zari Hassan mahususi kwa kongamano la wanawake katika biashara na ujasiriamali.

Licha ya kongamano hilo kuwa mahususi kujadili nafasi za wanawake walioko katika ujasiriamali lakini changamoto zinazowakabili, baadhi ya wanaume tajika walialikwa.

Mmoja wa wanaume walioalikwa kuhudhuria kongamano hilo ni msanii Samidoh.

Samidoh katika picha ambazo alizichapisha kwenye kurasa zake mitandaoni alionekana kupungwa pakubwa na furaha baada ya kukutana na mjasiriamali Zari Hassan, anayejitambua kama The Boss Lady.

Samidoh alisema kwamba ilikuwa furaha ya kupata nafasi adimu ya kuhudhuria mkutano wa wanawake katika biashara na ujasiriamali na kumsifia Zari kwa kile anachokifanya kuwaongoza wanawake wenza katika kujitegema kwa kujiingiza katika ujasiriamali.

“Jioni ya leo, nimejivunia kuwa na fursa nzuri ya kutumbuiza Wanawake katika Biashara Kenya Ilikuwa nzuri kushuhudia wanawake bora wakitunukiwa tuzo kwa ubora wao katika Biashara na kuwa na mwingiliano mzuri. Asanteni sana,” alichapisha Samidoh.

Awali tuliripoti kuwa Zari aliweza kuzungumzia mengi kuhusu familia yake ikiwemo mpango wa kuwafukuza wanawe wakubwa kutoka nyumba yake ili kujitafutia maisha mbali na yeye.

Pia mwanamama huyo aliweka wazi kwamba kuonekana kwake na Diamond mara kwa mara msanii huyo anapozuru Afrika Kusini hakuna maana yoyote kwamba watarudiana bali ni kutokana na urafiki wao na kiunganishi na milele baina yao – watoto.