Zari kuwafukuza vijana wake 3 wakubwa nyumbani, "Wameshakuwa watu wazima sasa!"

"Wanamiliki vyumba na magari, na wanahitaji kwenda. Wanahitaji tu kwenda. Kwa hivyo tunatumai kuwa hilo litapangwa mwaka ujao," alisema.

Muhtasari

• Zari ni mama wa watoto 5, watatu wakubwa wakiwa ni wale aliozaa na marehemu mumewe, Ivan Semwanga.

Zari Hassan na wanawe
Zari Hassan na wanawe
Image: Instagram

Mjasiriamali maarufu wa Uganda mweney makaazi yake Afrika Kusini, Zari Hassan amefichua mipango ya kuwafukuza vijana wake watatu aliozaa na marehemu mume wake kutoka nyumbani kwake ili kwenda nje kujitafutia maisha yao.

Zari alifichua mipango hii katika klipu moja ya TikTok akihojiwa ambapo alisema kwamba kwa sasa wanawe hao ni watu wazima ambao wanafaa kuanza kujitafutia maisha na sio tu kuendelea kulelewa na mama yao wakati wameshazidi miaka 18.

Zari alisema kwamba kinachomchochea Zaidi kuwafukuza nyumbani kwake ni baada ya klipu ya hivi majuzi ambayo iliwaonesha wakipigania nafasi ya kuegesha magari kila mmoja akitaka kuliegesha gari lake kwenye nafasi hiyo hiyo moja.

"Bado tunapigana kuhusu maegesho katika yadi yangu, lakini natumai, wavulana wangu watahama mwaka ujao. Wanamiliki vyumba na magari, na wanahitaji kwenda. Wanahitaji tu kwenda. Kwa hivyo tunatumai kuwa hilo litapangwa mwaka ujao," alisema.

Zari ni mama wa watoto 5, watatu wa kwanza ambao ni watu wazima sasa wakiwa wote ni wavulana aliozaa na marehemu mumewe Ivan Semwanga huku wadogo wawili akizaa na msanii Diamond Platnumz kati ya mwaka 2015 na 2018 kabla ya kuachana.

Kwa sasa, mama huyo anaishi na mpenzi wake mdogo, Shakib Lutaaya Cham ambaye walifunga ndoa ya kiislamu mwezi Aprili mwaka huu.