Mrembo avunja rekodi ya dunia ya Guiness kwa kukumbatia mti kwa mfululizo wa saa 15

Alilenga kufikia na kuvuka rekodi ya kudumu ya saa 10 na dakika 5 iliyowekwa na Adrienne Long mnamo Septemba 2020.

Muhtasari

• Alilenga kufikia na kuvuka rekodi ya kudumu ya saa 10 na dakika 5 iliyowekwa na Adrienne Long mnamo Septemba 2020.

Ariokot aweka rekodi ya dunia ya guinness.
Ariokot aweka rekodi ya dunia ya guinness.
Image: x

Mrembo wa Uganda hatimaye amefanikiwa kuweka rekodi ya dunia ya Guiness kwa kutumia muda mrefu Zaidi akiwa ameukumbatia mti.

Akianza harakati zake za kutafuta rekodi ya dunia tarehe 29 Desemba 2023, mrembo wa Uganda ambaye pia ni mwanaharakati wa mazingira, Faith Ariokot Partricia alikuwa tayari amejaribu kushinda rekodi hiyo hiyo tarehe 8 Desemba lakini alikumbana na changamoto chache zikiwemo hitilafu za kamera.

Mwanzilishi wa ‘Imani Katika Miti’ anadai analenga kuweka rekodi yake ya wakati katika kukumbatia miti kwa sababu anaamini kwamba “miti ni muhimu.”

"Nilijaribu Rekodi ya Dunia ya Guinness mnamo tarehe 8 Desemba 2023 kwa kukumbatiwa kwa mti mrefu zaidi na mtu binafsi. Ingawa nilivunja rekodi, Kamera yetu ilishindwa na ikakosa dakika za jaribio. Kwa sababu hii, nitakuwa nikijaribu tena rekodi hii tarehe 29 Desemba 2023. Ninafanya hivi kwa sababu Trees Matter na ninahitaji usaidizi wako ili hili lifanyike,” Ariokot alitweet tarehe 23 Disemba.

Akiwa amevalia fulana nyeusi na suruali ya kaki, jaribio la Ariokot lilianza asubuhi ya Desemba 29 katika Hoteli ya Mei 7 katika Jiji la Soroti.

Alilenga kufikia na kuvuka rekodi ya kudumu ya saa 10 na dakika 5 iliyowekwa na Adrienne Long mnamo Septemba 2020.

Haya yanajiri wakati ambapo Muganda mwingine, Mpishi Dorcus Bashema Kirabo, ambaye sasa anajulikana kama Mama D anaendelea kuongeza muda wa rekodi katika mbio za marathon za upishi ambazo alianza tarehe 10 Desemba 2023.

Ustahimilivu wa Ariokot tayari umevutia hisia za Waganda wengi wanaomfuata ili kuhakikisha anaandika jina lake katika rekodi za kimataifa.

Hata hivyo, Ariokot ambaye alisema alikuwa analenga saa 17 alilazimika kukatiza harakati hizo kunako saa 15 baada ya mingurumo ya radi kuanza.

“Nchi yangu. Watu wangu. Wapenzi wangu. Tulifanya. Tulivunja rekodi ya dunia ya saa 8:00. Tulipita muda tuliotarajia wa saa 13:00. Tulikuwa njiani kufanya angalau 17hours. Kisha radi ikapiga na hatukuwa na chaguo ila kusimamisha jaribio hilo. Saa 15 na dakika 19 haswa. Tumeweka rekodi mpya @GWR. Mimi ni mzima na niko nyumbani. Moyo wangu umejaa. Asante.”