Esther Musila na Guardian Angel waadhimisha miaka 2 katika ndoa

“Siku hii miaka miwili iliyopita, nilifunga ndoa na rafiki yangu mkubwa na kati ya hadithi zote za mapenzi ulimwenguni, hadithi yetu itakuwa ninaipenda zaidi." Musila aliandika.

Muhtasari

• “Tukitafakari juu ya safari yetu, kuna mambo 3 ambayo yatadumu daima; IMANI, UPENDO, na TUMAINI. Kubwa kwetu ni UPENDO." Musila alisema,

• Wawili hao wamekuwa wakionesha mapenzi yao hadharani licha ya kukashifiwa kutokana na utofauti mkubwa wa umri kati yao.

Wanandoa Musila na Angel
Wanandoa Musila na Angel
Image: Instagram

Msanii wa injili Guardian Angel na mpenziwe Esther Musila wamesherehekea miaka miwili tangu wafunge ndoa yao rasmi.

Musila kupitia ukurasa wake wa Instagram alishiriki msururu wa picha nzuri wakiwa pamoja na kusisitiza kwamba Angel ndiye mwanamume bora ambaye amemfaa kwa kila kitu katika kipindi cha miaka miwili pamoja.

Musila alisema kwamba katika hadithi za kimapenzi ambazo zitasimuliwa, bila shaka yao itajitokeza mbele kama hadithi bora, huku akisema kwamba msanii huyo alibadilisha kabisa mtazamo wake katika mduara wa mapenzi.

“Siku hii miaka miwili iliyopita, nilifunga ndoa na rafiki yangu mkubwa na kati ya hadithi zote za mapenzi ulimwenguni, hadithi yetu itakuwa ninaipenda zaidi. Hii imekuwa safari nzuri, na mimi bado ni bibi arusi wako, na wewe bado ni bwana harusi wangu. Bado ni honeymoon...” alisema Musila.

“Tukitafakari juu ya safari yetu, kuna mambo 3 ambayo yatadumu daima; IMANI, UPENDO, na TUMAINI. Kubwa kwetu ni UPENDO. MAPENZI YAMESHINDA!! Kila siku, ninakupenda zaidi kuliko siku iliyopita. Unawafanya Mr & Bibi waonekane rahisi sana....” aliongeza.

“Mume wangu mpendwa, ulifafanua upya maana nzima ya uandamani. Bado nashangaa jinsi unavyokaa vizuri katika ndoa yetu. Asante kwa kuwa chanzo cha daima cha furaha na nguvu. Heri ya kumbukumbu ya miaka kwetu! Nakupenda G ❤️❤️❤️.”

Wawili hao walipatana miaka michache iliyopita katika hafla moja na mapenzi yao yakaanza hapo hadi pale walipofunga ndoa ya faragha Janauri mwaka 2022.

Musila licha ya kupokea kashfa kutoka kila kona kwa kukubali kuingia katika mapenzi na mwanamume ambaye yeye [Musila] anamshinda kwa takribani miaka 20, bado hajawahi aibika kushiriki hadithi ya mapenzi yao hadharani.

Ama kwa kweli, mwisho wa siku mapenzi ndio hushinda!