KRG ajisifia jinsi alivyotendea haki mistari yake kwenye kolabo mpya na Konshens

“Nadhani katika wimbo huu nimejieleza vizuri kwa uwezo wangu katika mtindo wa dancehall, na pia nimewakilisha mtaa vizuri sijawaangusha masala" KRG alisema.

Muhtasari

• KRG pia alipata kujieleza Zaidi kwa nini anahisi wimbo huo na Konshens una utofauti wa ladha na nyimbo zingine nyingi ambazo amekuwa akizitoa.

KRG
KRG
Image: Facebook

Msanii KRG the Don amezindua ngoma yake ya kolabo ambaye amemshirikisha mkali kutoka Jamaica, Konshens.

Akizungumza na waandishi wa habari za mitandaoni wakati pia akisherehekea siku yake ya kuzaliwa jioni ya Jumatano, KRG alisema kuwa aliona ni wakati mwafaka wa kuachilia ngoma hiyo ambayo alidai iliwagharimu muda wa miaka 2 kuitayarisha.

“Kila kitu huwa nimepanga na unajua hii ni kolabo yenye imechukua kama miaka 2, si mmengoja sana? Tulifanya ngoma nyingine tukasikia ni kama haiku sawa tukatulia tukapanga tena tukafanya nyingine sasa hii ni ya tatu. Ndio tukasema sasa hii tuko sawa nayo wacha tuwapige za macho,” KRG alisema huku akiisifia ngoma hiyo.

Msanii huyo alisema kufanya kolabo na Konshens ni hatua nyingine kubwa Zaidi katika taaluma yake ya muziki, kwani imemfungua akili kuona kwamba anaweza kuchukulia taaluma hiyo kwa umakini mkubwa kama biashara.

“Hii ni hatua nyingine katika taaluma yangu ya muziki kwa sababu kwa muda mrefu mimi nilikuwa najua mimi ni mkali lakini sikuwa tayari kufanya muziki muda wote kama biashara lakini sasa huu mwaka nimekuja kivingine, nitatenganisha wavulana na wanaume,” alisema kwa kujitapa kama ilivyo kawaida yake.

KRG pia alipata kujieleza Zaidi kwa nini anahisi wimbo huo na Konshens una utofauti wa ladha na nyimbo zingine nyingi ambazo amekuwa akizitoa.

“Nadhani katika wimbo huu nimejieleza vizuri kwa uwezo wangu katika mtindo wa dancehall, na pia nimewakilisha mtaa vizuri sijawaangusha masala kwani chenye mtakaka kusikiliza sasa hivi na wave ya sasa ndio iko kwenye huo wimbo na vile nimedeliver najua nimefanya fiti lakini pia video tulifanya nzuri na nadhani hiyo ndio kitu inafnaya ngoma ikuwe ya kipekee,” alisema.