Sonko:Kama kuna mrembo nilipachika mimba kibahati mbaya nikiwa makanga njoo DNA

Sonko alisema yeye ni mtu ambaye anapenda maisha ya uwazi na uwajibikaji na lengo lake kuitisha DNA kwa yeyote anayemsingizia ni kutaka kujua idadi kamili ya wanawe na wajukuu wake pia.

Muhtasari

• "Kama kuna mrembo nilishiriki mapenzi bahati mbaya nikiwa shule au makanga Buruburu ama wakati nikienda korti moja kwenda nyingine ule wakati nikiwa jela Shimo La Tewa au Kamiti njoo tufanye DNA," Sonko alisema.

Mike Sonko.
Mike Sonko.
Image: X

Mfanyibiasha ambaye pia aliwahi kuwa mbunge na gavana wa Nairobi Mike Sonko ameonyesha utayarifu wake kufanya vipimo vya DNA na mwanamke yeyote ambaye anahisi kuwa aliwahi kushiriki mapenzi na yeye na kupata mimba yake.

Sonko kupitia ukurasa wake wa Twitter, aliandika ujumbe mrefu akiisifa familia yake kubwa ikijumuisha wanawe wa kuwazaa pamoja na wengine wengi ambao amekuwa akiwaasili.

Akisema kuwa kila mtu ana jana mbaya, mfanyibiashara huyo mkwasi aliweka wazi kwamba anajijua mambo na matendo ambayo alikuwa akishiriki kipindi hajakuwa mwanasiasa.

Sonko alisema milango i wazi kwa mwanamke yeyote ambaye kwa bahati mbaya huenda alimpa mimba na kusahau enzi akiwa makanga wa magari ya BuruBuru au akiwa shule au nyakati anahamishwa kutoka gereza moja kuelekea nyingine, basi amfuate na mtoto huyo kwa ajili ya uthibitisho kamili wa baba.

“Kwa vile kila mtu ako na zamani yake na mimi ninapenda kuwa muwazi, kama kuna mrembo nilishiriki mapenzi bahati mbaya nikiwa shule au makanga Buruburu ama wakati nikienda korti moja kwenda nyingine ule wakati nikiwa jela Shimo La Tewa au Kamiti na ukapata mimba bahati mbaya na mtoto wako ameoa au ameolewa akazaa hebu kimbia haraka tufanye DNA nitalipia. Nataka kujua niko na wajukuu wangapi katika umri huu,” Sonko alisema.

Ikiwa siku ya Alhamisi ambayo wengi hutafakari maisha yao ya nyuma, Sonko alionesha furaha yake ya kufanywa babu katika umri wake mdogo kutokana na uzao wa mabinti zake.

“Wasichana wangu nao wamenifanya nikakua one of the youngest proud grandpas today. Saumu, ambaye ana umri wa miaka 30, ni mama wa watoto wawili Sasha (miaka 6) na Ummi (miaka 3). Salma, ambaye ana umri wa miaka 27, pia ni mama wa watoto wawili pamoja na Ermias (miaka 4) na Talha (miaka 3),” Sonko alitamba.