"Siwezi kutukana kilema!" KRG ajibu baada ya Stevo Simple Boy kumuita 'video vixen'

“Yaani unajua sasa hivi kuna wave inatembea, watu wengi washajua kwamba ukitaka kuwa maarufu, tukana KRG, akikutusi tu, umeshafanikiwa, sasa hiyo energy sitaki kabisa,” alisema.

Muhtasari

• Miezi 10 iliyopita, KRG alimtaja Stevo kama kinyago baada ya rapa huyo wa Freshi Barida kusema kwamba hakuwa anamjua KRG ni nani.

Stevo na KRG
Stevo na KRG
Image: Facebook

Siku chache baada Stevo Simple Boy kumdhalilisha KRG the Don kwa kumtaja kuwa si msanii bali ni vixen wa kwenye video, msanii huyo wa dancehall amemjibu.

KRG katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini, alipoulizwa ana lipi la kusema baada ya Stevo kumuita vixen, KRG alisema kwamba hayuko tayari kumjibu Stevo kwa matusi.

Msanii huyo anayejitapa kama tajiri Zaidi kimuzki humu nchini alisema kwamba ameamua kutojibizana na rapa huyo wa Kibera kwa vile anajua yeye [Stevo] anatafuta njia ya kuzungumziwa mitandaoni kwa kuliburura jina la Bughaa.

“Sitaki kutukana kilema, siwezi mtukana,” KRG alisema.

“Yaani unajua sasa hivi kuna wave inatembea, watu wengi washajua kwamba ukitaka kuwa maarufu, tukana KRG, akikutusi tu, umeshafanikiwa, sasa hiyo energy sitaki kabisa,” alisema.

Stevo alikuwa anazungumzia tamko la mbunge Jalang’oo kumweka mbele ya KRG katika tasnia ya marapa walio juu nchini.

Alipoulizwa kama anaweza kufanya ngoma na KRG, Stevo alijibu;

“KRG si msanii, yeye ni vixen tu. Hata kama unafanya kolabo na msanii kutoka Jamaika, mimi sijali, wewe ni vixen, tafuta siku moja uje ukuwe kama vixen kwenye muziki wangu.”

Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kupapurana.

Miezi 10 iliyopita, KRG alimtaja Stevo kama kinyago baada ya rapa huyo wa Freshi Barida kusema kwamba hakuwa anamjua KRG ni nani.

“Sio kwa ubaya ama nini, lakini huyu KRG ni nani nimetajwa sana kwenye Instagram, na mbona tunapiganishwa kimuziki?” Stevo Simple Boy aliuliza kwa kejeli.

“Sasa wewe Stevo Simple Boy, chenye naweza kufanyia ni kukupeleka pale kwenye shamba langu, nikuvalishe kanga ukuwe kama kinyago. Kwa sababu sura yako inatisha sana, usijaribu kujilinganisha na mtu mtanashati kama mimi,” KRG alijibu kwa dharau.