Khaligraph awashauri wanablogu kuwekeza kwenye kamera nzuri ili kumu'interview

"Usifikirie kuwa ninapokuja kwenye mahojiano yako wewe ndio unanipa jukwaa. Mimi ndiye ninakupa jukwaa ili kuboresha, weka kamera bora."

Muhtasari

• Msanii huyo alitania kwamba kwenda mbele atakuja kuanza kuwachuja wanablogu ambao hawako serious kwa kazi zao.

Khaligraph Jones.
Khaligraph Jones.
Image: Screengrab

Rapa namba moja kwa muda wote nchini Kenya, Khaligraph Jones amewajia juu wanablogu kwa kile anahisi kwamba wengi wao wanaripoti habari za kupotosha kuhusu wasanii na watu maarufu.

Akizungumza na SPM Buzz, Jones aliwatuhumu wanablogu kwa kile alisema kwamba wengi wao hawako sawa kitaaluma akisema hata wengine wanatumia vifaa duni ilmradi tu kurekodi na kuchapisha taarifa zisizo sahihi kuhusu watu maarufu.

“Mnabooh. Ninaamini nyinyi mnafanya kazi yenu na ninaheshimu kila mtu anayefanya kazi hapo. Ni kazi yako kublogi na kuchapisha kuhusu hadithi lakini kabla ya kuweka taarifa fulani thibitisha habari hiyo.”

Khaligraph alisema kwamba wengine wanatafuta unga kwa kucnapisha taarifa za kuwachafulia watu majina na picha bila kujua kwamba wengine ni watu na familia zao.

“Unapata wengine wanaeka information mbaya kama mimi, sisi ni watu tuko na familia wengine na ukifanya tu kitu ndio upate traction kwa nini yako, vitu kama hizo ni vitu mbaya. Hatujaribu jambo hili sisi ni wataalamu katika hili na nyinyi mnatakiwa kuwa weledi upande wenu, kabla ya kutuma chochote hakikisheni taarifa hizo kwa sababu si poa saa injini,” alisema.

Msanii huyo alitania kwamba kwenda mbele atakuja kuanza kuwachuja wanablogu ambao hawako serious kwa kazi zao.

Alisema kwamba wanablogu kama wanathamini kazi zao wanafaa kuwekeza katika vifaa bora, akitania kwamba atakuja kuanza kutakaa kuhojiwa na mwanablogu ambaye hana kamera za hali ya juu kama zile ambazo wasanii kama Jay Z wanahojiwa nazo.

“Mimi kwanza sipendi hii kamera mnatumia, mnunue kamera ingine sahi mnafaa kuniweka kwa kamera kama za akina Jay Z coz Khaligraph yuko mbele yako, hili ni jina kubwa,” alisema kwa mzaha.

"Usifikirie kuwa ninapokuja kwenye mahojiano yako wewe ndio unanipa jukwaa. Mimi ndiye ninakupa jukwaa ili kuboresha, weka kamera bora. Ila nakutania tu,” alisema zaidi.