Zuchu awataka warembo wa kwao Zanzibar kuchangamkia fursa ya ku'date na Dvoice

Zuchu anataka warembo wa kisiwa cha Zanzibar kuteka anga za Wasafi kwa njia zote, kwani yeye tayari ameshajinafasi si tu kama msanii bora wa kike wa lebo lakini pia mpenzi wa bosi wa lebo, Diamond Platnumz.

Muhtasari

• Aliwataka wamtunze vizuri Dvoice wakati wa shoo yake na kuwaasa kwamba angependa Dvoice arudi Dar es Salaam na mmoja wao kama mpenzi wake.

DVOICE.
DVOICE.
Image: Facebook

Msanii Zuchu ambaye anatokea katika visiwa vya Zanzibar amewapa changamoto warembo wa kutoka kisiwa hicho kuwahi fursa adimu ya kuchumbiana na msanii mpya wa lebo ya WCB Wasafi, Dvoice.

Kupitia kwa Instagram yake, Zuchu alipigia debe shoo ya Dvoice ambayo itafanyika katika kisiwa hicho tarehe 27 mwezi huu na kuwataarifu warembo wa kwao huko kwamba msanii huyo bado yuko bila mpenzi, kwa hiyo wasiache fursa hiyo iwatokee puani wakiangalia.

Aliwataka wamtunze vizuri Dvoice wakati wa shoo yake na kuwaasa kwamba angependa Dvoice arudi Dar es Salaam na mmoja wao kama mpenzi wake.

“Zanzibar mdogo wetu anakuja tarehe 27 mwezi huu, tafadhali mtunze vyema na pia jueni yuko single. Kwa hiyo msiniangushe, arudi na wifi tumuwahi mapema,” Zuchu alipiga debe.

Kwa tafsiri ya haraka, Zuchu anataka warembo wa kisiwa cha Zanzibar kuteka anga za Wasafi kwa njia zote, kwani yeye tayari ameshajinafasi si tu kama msanii bora wa kike wa lebo lakini pia mpenzi wa bosi wa lebo, Diamond Platnumz.

zuchu, d voice
zuchu, d voice

Zuchu na Diamond wamekuwa katika mapenzi bairid-moto ikiwa ni kuachana na kurudiana baada ya muda mfupi.

Wawili hao wamekuwa wakiwachanganya mashabiki wao kwa penzi lao la mitandaoni, ambalo kwa wakati mwingine wanaachia jumbe za kuonesha kwamba wameachana lakini muda mfupi baadae tena wanaonekana pamoja.

Mapema wiki iliyopita, Diamond aliwashangaza wengi baada ya kuandika kwamba yuko single na hahitaji mpenzi tena.

Hili liliwafanya wengi kuhisi kwamba Zuchu keshaachika lakini saa chache baadae, msanii huyo wa WCB alikwenda kwenye mitandao tena na kudai kwamba hayuko single bali penzi lake na mpenzi kutoka kisiwa cha karafuu – Zuchu – bado ni wake na hawatoachana muda wowote hivi karibuni.