Gloria Ntazola achukizwa na wanaume wanaotumia filters za Snapchat na kushinda TikTok

Ntazola alisema kwamba kwake, tafsiri ya mwanamume kamili ni yule ambaye ni mwenye taaluma nzuri kama udakrari, rubani au hata mhandisi.

Muhtasari

• “Wanaume wa siku hizi, eti nitumie maua, mara tap tap kiwambo sijui nini…nani anachumbia wanaume hawa wa TikTok? Heri nichumbiane na mwizi wa kuiba kwa bank kuliko hawa wa TikTok." Ntazola alisema.

Ntazola
Ntazola

TikTok Gloria Ntazola aliyepata umaarufu wa ghafla shukrani kwa klipu yake akikorofishana na askari wa kaunti ya Nairobi – Kanjo – ameonesha kukerwa kwake na wanaume ambao wanaiga tabia za kike katika mitandao ya kijamii.

Ntazola kupitia instastories zake alitenganisha mpunga na mchele na kusema kwamba kuna wanaume wengi ambao wamepoteza uanaume wao kisa mitandao ya kijamii.

Mrembo huyo ambaye ni mjasiriamali wa vipodozi na bidhaa za urembo alisema kwamba anachukizwa na wanaume wanaopiga picha kwa kutumia filters za Snapchat huku wengine wakishinda siku nzima kwenye mtandao wa TikTok kuomba zawadi za maua.

Ntazola alisema kwamba kwake, tafsiri ya mwanamume kamili ni yule ambaye ni mwenye taaluma nzuri kama udakrari, rubani au hata mhandisi.

“Wakati mwingine naangalia vitu katika mtandao huu na najipata naaibika kweli kwa niaba ya kila mtu akiwemo mhusika mwenyewe. Kwa nini mwanamume mzima anaweza kutumia filters za Snapchat? Mbona uko katika TikTok ukiomba maua? Wanaume kamili wanafaa kuwa madaktari, wahandisi na marubani. Ondoka TikTok na utafute kazi nzuri ya kufanya,” Ntazola alipiga tantarira.

Mrembo huyo alizidi kuwakandamizia wanaume wa siku hizi akisema kwamba wengine wanashinda kwenye mtandao wa TikTok kutafuta wapenzi.

Ntazola alisema kwamba hakuna mrembo mwenye akili timamu anayeweza kuchumbiana na mwanamume wa TikTok, akisema kwamba wezi wa huku nje wanaweza kuwa wanaume bora Zaidi kuliko wanaume wa TikTok.

“Wanaume wa siku hizi, eti nitumie maua, mara tap tap kiwambo sijui nini…nani anachumbia wanaume hawa wa TikTok? Heri nichumbiane na mwizi wa kuiba kwa bank kuliko hawa wa TikTok. Huwezi kuwa unalala nyumbani kutoka Jumatatu hadi Jumatatu ukiomba watu wakutumie maua, hiyo haiwezi, tafuteni kazi kama kweli wewe ni mwanamume kamili,” aliendelea kutoa mzomo.

Ntazola alizidi kutupa bomu gizani akisema kwamba baadhi ya watu wanajihisi kuwa ni maarufu kwa kupata wafuasi wachache katika mtandao wa TikTok.

Kwa mujibu wa Ntazola, hakuna mtu anayejali kama wewe ni celeb bila pesa, akisema kwamba mtu celeb pekee mwenye uwezo wa kutamba na kuvimba ni rais wa nchi tu.

“Kuwa na wafuasi kiasi kwenye TikTok hakukufanyi kuwa celeb, niamini mimi hakuna mtu anayejali kuhusu hilo. Wewe sio celeb, celeb ni rais wa nchi pekee, hatuwezi kukutafuta kupitia google na hatuwezi taka kujua salio katika benki yako kwa sababu hata huna akaunti kwa hiyo tulia tu na upunguze matarajio yako,” Ntazola aliwaziba midomo wenye mikogo.