Mimi napenda wanaume wachapakazi, sijali kama ni maskini au tajiri – Georgina Njenga

Georgina anaelezea mwanamume wa kumpenda siku chache baada ya aliyekuwa mpenziwe Baha naye kufunguka kuhusu mwanamke ambaye angependa kuchumbiana naye.

Muhtasari

• Njenga alisema kwamba ladha yake kwa mwanamume kamili ni yule anayejituma, bila kujali kama ni maskini au tajiri.

Georgina Njenga
Georgina Njenga
Image: Instagram

TikToker Georgina Njenga amefunguka kuhusu mwanamume ambaye angependa kuchumbiana naye, siku chache baada ya aliyekuwa mpenzi wake, Baha Machachari naye kuorodhesha vigezo atakavyoviangalia kwa mpenzi wake mpya.

Njenga kupitia Instagram stori alikuwa anamjibu shabiki mmoja aliyemuuliza kama angependa kuchumbiana na mwanamume maskini au tajiri.

Njenga alisema kwamba ladha yake kwa mwanamume kamili ni yule anayejituma, bila kujali kama ni maskini au tajiri.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba kwake, muda wote atamchagua mwanamume anayemuona kuwa anajituma na ni mchapakazi.

“Mimi nitachagua mwanamume mchapakazi kwa asilimia 100. Kwa wale maskini, kama kweli ninaweza ona maendeleo katika kujituma kwake mbona nisimkubali? Wanaume wanaofanya kazi kwa bidii hunipunga pakubwa,” Njenga alisema.

Ungamo la Njenga linakuja siku chache baada ya babydaddy wake waliyeachana mwaka jana, Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari kuonekana kwenye video akizungumzia kuhusu mwanamke ambaye angependa kuchumbiana naye baada ya penzi lake na Njenga kubuma.

Baha alisema kwamba kinyume na siku za nyuma, safari hii hatoweza kuzingatia katika muonekano wa nje au sura bali atazingatia Zaidi katika mrembo atakayempa Amani ya nafasi lakini pia mrembo mwenye akili.

"Sitafuti chochote cha mwili ingawa kinaweza kucheza. Ninataka mtu mwenye akili, na mwaminifu na anapaswa kuwa nafasi yangu salama. Ninataka mtu ambaye anaweza kunipa vibe vya amani,” alisema.

Mnamo Julai 2023, habari ziliibuka kuhusu kutengana kwa Baha na mamake mchanga Georgina Njenga, na hivyo kuashiria mwisho wa uhusiano wao wa ndani na nje kupitia uamuzi wa pande zote.

Wakati wa kipindi cha Maswali na Majibu kwenye Instagram, Georgina alizungumzia utengano huo wakati shabiki alipouliza kuhusu uhusiano wake na Tyler Mbaya.

Mgawanyiko huo ulitokea muda mfupi baada ya Baha kuzua utata kwenye mitandao ya kijamii kwa shutuma za ulaghai.