Zari: Nikiwa mdogo nilikuwa na ndoto ya kuolewa na mtu tajiri lakini nikagundua sio rahisi

“Nimejifunza kugawa muda wangu katika mambo muhimu, nampa kipaumbele sana mume wangu, nawapa muda watoto wangu, na pia natenga muda kwa ajili ya biashara" Zari alisema,

Muhtasari

• Mama huyo wa watoto watano alifichua kwamba ni kweli akiwa mtoto ndoto yake kuu ilikuwa ni kulala na kuamka na kuposwa na mwanamume tajiri.

Zari
Zari
Image: Instagram

Mjasiriamali Zari the Bosslady amefunguka mengi kuhusu maisha yake kwa jumla tangu utotoni na vitu ambavyo anavipa thamani na muda mwingi katika maisha yake.

Zari katika kikao na BBC Swahili huko London, aliketi kwenye kiti cha moto na kuulizwa maswali matano ya moto ambayo aliyajibu kwa ufasaha.

Moja ya maswali ambayo Zari aliulizwa ni kuhusu maisha yake akiwa mdogo kama alikuwa anayatamani maisha ya kifahari ambayo ako nayo kwa sasa.

Mama huyo wa watoto watano alifichua kwamba ni kweli akiwa mtoto ndoto yake kuu ilikuwa ni kulala na kuamka na kuposwa na mwanamume tajiri.

Hata hivyo, Zari alifichua kwamba haikuwa rahisi kama alivyokuwa anafikiria, kwani ilimbidi kuamka kutoka ndotoni na kuanza kufanya kazi.

Alifichua kwamba alifanya kazi duni kwa Zaidi ya maika 20 kabla ya kuyapata maisha ambayo anajivunia sasa hivi, huku pia akifutilia mbali dhana kwamba mali nyngi alirithi kutoka kwa marehemu mum wake.

“Mimi nilikuwa nadhani kwamba nitaamka, niolewa na mwanamume tajiri, navaa dhahabu ghali… lakini nikagundua kwamba sio rahisi. Huo ndio wakati niligundua kwamba kweli nahitaji maisha mazuri lakini lazima niyafanyie kazi,” alisema.

Mjasiriamali huyo alifunguka kwamba kilichompa msukumo Zaidi kufanya kazi bila kuchagua ni dhana kwamba hakuwa anatoka katika familia nzuri.

“N hicho kilinipa motisha kwamba sitoki katika familia nzuri kihivyo, kwa hiyo lilikuwa ni jukumu langu, nikasema wakati nitarudi nitafanya bidii Zaidi,” aliongeza.

Katika swali la ni vipi anaugawa muda wake, Zari alisema kwamba kwa sasa vitu ambavyo anavipa muda mwingi ni mume wake na watoto wake.

“Nimejifunza kugawa muda wangu katika mambo muhimu, nampa kipaumbele sana mume wangu, nawapa muda watoto wangu, na pia natenga muda kwa ajili ya biashara. Yote kwa yote ni namna ambavyo ninapangilia mambo yangu, usipopanga mambo yako kwenye maisha vizuri basi kila kitu hakitoenda sawa,” Zari alijibu.

Kuhusu siri ya mafanikio yake, Zari alirudia pale pale kwamba muda wote anawashauri watu kuanza chini, na kile kidogo walichonacho.

“Mimi huwa nasema, na nitarudia tena, anza na hatua ya chini. Huwa nashangaa watu wanaodhani kwamba unafaa tu kuenda juu mara moja. Hapana, hiyo haiwezekani, watu wanaofanya hivyo ni wachache sana na ni wale walioteuliwa pekee. Ukiangalia safari ya maisha yangu nimefanya kazi kwa Zaidi ya miaka 20 na hizo ndizo hatua ndogo. Kuna muda ukifika ukiangalia nyuma ulikotoka unasema eeh kumbe nimetoka mbali hivi, kwa hiyo anza na hatua za chini,” Zari alishauri zaidi.