Nilitaka kujiua baada ya mamangu kufa - Lulu Diva, msanii wa Bongo Fleva (video)

" Kwa sababu mimi mamangu alikuwa naweza nikasema ni mtu tofauti kabisa akisema mimi nampenda mamangu. Mimi mamangu alikuwa ni Zaidi ya rafiki kabisa,” Diva aliongeza.

Muhtasari

• Akizungumza na mwanablogu mmoja, Diva alisema amepitia maisha magumu sana na mama yake ndiye alikuwa nguzo pekee ya upendo.

Afichua kuwazia kujiua baada ya mama yake kufa
LULU DIVA// Afichua kuwazia kujiua baada ya mama yake kufa
Image: FACEBOOK//LULU DIVA

Msanii wa kike wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka makubwa aliyoyapitia baada ya kifo cha mama yake.

Akizungumza na mwanablogu mmoja, Diva alisema amepitia maisha magumu sana na mama yake ndiye alikuwa nguzo pekee ya upendo, kwani alipofariki, Diva alijihisi mpweke kiasi kwamba akatathmini kujitoa uhai pia katika kile alisema alihisi hakuna aliyekuwa anampenda kama mama yake.

“Mimi nimepitia maisha ambayo yamenifanya nimekuwa very very strong woman kiasi cha kwamba kuna muda, trust me nilitaka kujiua. Yaani hamna kipindi ambacho nilata kuondoka duniani kwa sababu sioni raha ya kutaka kuishi duniani kama mamangu hayupo,” Diva alisimulia.

“Nilikuwa sioni raha ya kukaa na watu tena. Kwa sababu mimi mamangu alikuwa naweza nikasema ni mtu tofauti kabisa akisema mimi nampenda mamangu. Mimi mamangu alikuwa ni Zaidi ya rafiki kabisa,” Diva aliongeza.

Pia aliweza kuzungumza kuhusu mipango yake ya ndoa na kusema kwamba hilo halimpi taabu wala kumkosesha usingizi, lakini pia hakuweza kufutilia mbali uwezekano wa kuingia katika ndoa wakati mmoja nyota ya jaha ikisimama upande wake na kumuangazia nuru.

“Yaani siko desperate na ndoa eti kwa sababu sijaolewa eti sina raha juu sina mume, hapana. Nakula, naishi na napendeza, kwa hiyo ndoa kama nimejaaliwa nitapoa. Kama kikombe cha ndoa ni changu, kitanijia. Kiukweli sina haraka sana na ndoa wala yaani si kitu changu ninaweza nikasema kwamba sasa hivi kinanifanya kuninyima usingizi, siko desperate,” Diva aliongeza.