Crazy Kennar ajibatiza kuwa 'mtu mbunifu zaidi aliye hai' na kutaka kusimuliwa vitabuni

“Subiri hadi upate sifa kutoka kwa mashabiki wako! Wewe sio mcheshi kama unavyofikiria. Ni vile tunajua ni unga unatafuta ndio maana we find you hilarious!” Towett Cheruiyot alimwambia.

Muhtasari

• “Hapana kaka ...Umepata wasikilizaji wanaokuunga mkono. Lakini hapo kwa kuwa genious zii. Badilisha au uangamie,” Sir Carlos Wenga alimwambia.

Crazy Kennar.
Crazy Kennar.
Image: FACEBOOK

Mchekeshaji Crazy Kennar amevutia maoni mseto katika mtandao wa X, awali ukijulikana kama Twitter baada ya kujidai kwamba yeye ndiye mtu mbunifu Zaidi aliyewahi kuishi.

Kennar alianza kwa kujisifia kuwa akili na ubongo wake unafanya kazi kama mashine ambayo inaona vitu kutoka kwa pembe tofauti za kimaisha na papo hapo kuibuka na ucheshi ambao huwafurahisha watu.

Mchekeshaji huyo ambaye alianza kufanya kazi kama mtu binafsi mwaka jana baada ya kusambaratika kwa kundi lake alitoa wito kwa waandishi wazuri kuchukua fursa hiyo na kuisimulia hadithi yake katika miswada yao ya uandishi.

Alikwenda hatua Zaidi na kupendekeza mada kuu ya kitabu hicho ambacho kitaandikwa kumhusu.

“Akili yangu ni kama mashine ya ubunifu, naona mawazo kutoka sehemu zote za eneo linalowezekana la fikira, naona hadithi, naona utani, naona bodi za hadithi, naona mistari ya kumbukumbu, naona ulimwengu wa filamu na TV katika fremu za sekunde 60. Mtu anapaswa kuandika kitabu juu yangu. Mada: The Most Creative Man Alive,” Kennar alisema.

Hata hivyo, watumizi wa X wale wale ambao humsifia na kumhongera pindi anapoachia video zake za kuchekesha walimshukia kwa kumponda kuwa hangestahili kujipiga kifua bali angesubiri watu wenyewe wamtambue kwa njia hiyo.

“Subiri hadi upate sifa kutoka kwa mashabiki wako! Wewe sio mcheshi kama unavyofikiria. Ni vile tunajua ni unga unatafuta ndo maana we find you hilarious! Lakini ungekuwa unafanya hivyo hadi miaka ya 40 lazima ubadilike kidogo,” Towett Cheruiyot alimwambia.

“Hapana kaka ...Umepata wasikilizaji wanaokuunga mkono. Lakini hapo kwa kuwa genious zii. Badilisha au uangamie,” Sir Carlos Wenga alimwambia.

“Kunakuwaga na wakati mwanaume anahisi ni bora kuliko mtu yeyote..maringo yanaingia...nenda kwa makini...Sanaa hainaga aliye bora,” DJ Swanky Vybz aliongeza.

“Kuhisi kama mtu mbunifu zaidi aliye hai ni nzuri! Kumbuka tu, kiburi huja kabla ya anguko. Kaa mnyenyekevu, endelea kuunda, na acha kazi yako ijisemee yenyewe,” Cjay Chege alimshauri.

Una maoni yepi kuhusu Kennar kujiita mtu mbunifu Zaidi aliye hai?