Eric Omondi: Niliwahi kula 50K ya mtu alinitumia akitaka nimsaidie kuingia iluminati

“Nikamwambia nitakusaidia uingie iluminati lakini usiambie mtu. Kuingia unalipa 100k lakini kwa sasa nataka unitumie 50k, utakuja na mbuzi rangi nyeupe na 25k..." Omondi alihadithia.

Muhtasari

• "Sababu ilifanya nikule pesa za huyo kijana ni kwa vile alisisitiza kuingia iluminati kupitia kwangu,” alisema.

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: Facebook

Mwanaharakati Eric Omondi amenyoosha maeleoz kuhusu uvumi kwamba yeye ni mwanachama wa iluminati.

Katika mahojiano na mwanablogu Trudy Kitui, Omondi alifunguka kwamba hayuko iluminati lakini watu wengi kwa muda wamekuwa wakimdhania kuwa mwanachama wa kundi hilo, jambo ambalo si kweli.

Omondi alisema kwamba uvumi huo ulianza kipindi akiwa mchekeshaji kwenye kipindi cha Chruchill.

 Alihadithia hadithi moja jinsi alipigiwa simu na mtu asiyemjua na kumtaka kumsaidia kujiunga na chama cha iluminati.

Omondi alijaribu kumkataza mtu huyo lakini alisisitiza kiasi kwamba Omondi alimtaka kutuma pesa ili kumsaidia kuingia lakini akala hilo hela na kumwambia mtu huyo kwamba ni mjinga.

“Huo uvumi umekuwepo tangu nikiwa Churchill Show. Mtu alinipigia simu mchana na kunitaka nimsaidie kuingia iluminati. Nikamwambia sijui iluminati ni nini. Nikamwambia siko. Akanipigia simu usiku tena akisisitiza nimsaidie kuingia iluminati,” Omondi alielezea.

“Nikamwambia nitakusaidia uingie iluminati lakini usiambie mtu. Kuingia unalipa 100k lakini kwa sasa nataka unitumie 50k, utakuja na mbuzi rangi nyeupe na 25k halafu nitakwambia venye utafanya. Na alituma. Pesa iliingia kwa hii simu yangu. Kama kuna pesa nishawahi kula ni hiyo. Akanipigia simu nilishika mara 2 nikamwambia wewe ni mjinga sana. Baadae nilimblock,” Omondi aliongeza.

Mwanaharakati huyo ambaye anasemekana kuwazia kujiunga kwenye siasa aliwashauri vijana kujituma kwa kile wanachokifanya bila kufikiria kwamba kuna mwanya wa iluminati wa kuwasaidia kufanikiwa kimaisha bila jitihada.

“Watu lazima wafanye kazi. Iluminati eti inakuwa nini. Sababu ilifanya nikule pesa za huyo kijana ni kwa vile alisisitiza kuingia iluminati kupitia kwangu,” alisema.