Mwanamume ni kama jogoo, hakuna jogoo haparamii kuku wa jirani – Inspekta Mwala (video)

“Mimi niko na familia [lakini kwa idadi ya wanawake], wala usijali. Unajua mwanamume ni jogoo. Hakuna jogoo ambaye haparamii kuku wa jirani,” Mwala alisema.

Muhtasari

• Kuhusu idadi ya watoto, Mwala alisema kwamba kwa tamaduni za Kiafrika, watoto hawahesabiwi na hivyo kudinda kufichua idadi kamili ya wanawe.

• “Wachana nayo, watoto hawahesabiwi, sisi ni Waafrika.”

Inspekta Mwala
Inspekta Mwala
Image: Facebook

Mchekeshaji wa muda mrefu Inspekta Mwala amejibu kuhusu idadi ya wanawake anaowamiliki katika maisha yake.

Licha ya kuonekana kuwa na umbile dogo kimwili, wengi aghalabu humchukulia kuwa mtoto lakini Mwala katika mahojiano kwenye runinga ya NTV Kenya kwenye kipindi cha Masogora, alifichua kwamba yeye ni mwanamume kamili mwenye familia yake.

Mchekeshaji huyo hata hivyo hakuweza kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu idadi ya wanawake anaowamiliki lakini alijificha nyumba ya nadharia kuwa mwanamume ni kama jogoo ambaye hawezi kuwasaza kuku wa kike wa jirani.

“Mimi niko na familia [lakini kwa idadi ya wanawake], wala usijali. Unajua mwanamume ni jogoo. Hakuna jogoo ambaye haparamii kuku wa jirani,” Mwala alisema.

Kuhusu idadi ya watoto, Mwala alisema kwamba kwa tamaduni za Kiafrika, watoto hawahesabiwi na hivyo kudinda kufichua idadi kamili ya wanawe.

“Wachana nayo, watoto hawahesabiwi, sisi ni Waafrika.”

Mwala ambaye amekuwa kwenye tasnia ya uigizaji na ucheshi kwa miaka mingi alifichua kiasi kikubwa cha hela ambacho aliwahi shika mwa mkupuo.

“Nimeshawahi pata hadi milioni 2 kwa mara moja pap! Hata hivyo hii kazi si eti ina pesa nyingi za kukidhi mahitaji yako maisha yako yote jinsi unavyotaka kukaa,  kwenye hii taaluma tunajiendeleza na riziki za kando, pengine kufanya matangazo ya biashara mahali, kuwa MC kwenye harusi mahali… na nyingine,” Mwala alifunguka.

Tazama video hiyo hapa chini;