Otile Brown avunja kimya saa chache baada ya KRG kumtuhumu kwa kukosa fadhila

"Mimi siko hapa kwa sababu tu Niko talented but ni kwa sababu na heshima, baraka za Mungu na nazilinda kwa sababu najua Mungu hapendi watu wasio na fadhila,” aliongeza.

Muhtasari

• Hata hivyo aliwaonya wale aliowahi kuwasaidia na wakaenda kulaza damu kwamba hatowapa msaada kwa mara ya pili tena.

Otile Brown
Otile Brown
Image: Instagram

Otile Brown amevunja kimya chake baada ya KRG kumtupia maneno makali mitandaoni akisema kwamba msanii huyo wa albamu ya Grace hana fadhila.

Kupitia instastory yake, Otile aliandika ujumbe akiwalenga wasanii ambao amewahi kuwasaidia kutusua lakini wakaenda na kulaza damu.

Hii ni licha ya KRG kudai kwamba msanii huyo hajawahi msaidia msanii yeyote wala hana fadhila kwa watu ambao walimshika mkono na kumtambulisha vichochoro vya Nairobi wakati alikuwa mbichi kwenye tasnia ya muziki.

Brown alisema kwamba yeye kwa wakati mrefu amekuwa akiwasaidia wasanii hata kwa ushauri mpaka wengine wakambandika jina ‘mtu wa ushauri’.

Hata hivyo aliwaonya wale aliowahi kuwasaidia na wakaenda kulaza damu kwamba hatowapa msaada kwa mara ya pili tena.

"Nikikusaidia kukua na ukafeli kwenye tasnia hii iliyopo usianze kucheza michezo ya lawama…nimeona wengi mnapapasa mfuko baada ya kuwashauri na kuwapa mchezo sana..adi mnaniitaga" msee ma ushauri" unapofanya mzaha.”

“"Mkisha sota una expect urudi nikupokee mride kwa wave yangu tena just to go and fumble it again. Mimi siko hapa kwa sababu tu Niko talented but ni kwa sababu na heshima, baraka za Mungu na nazilinda kwa sababu najua Mungu hapendi watu wasio na fadhila,” aliongeza.

Akionekana kulenga mkuki wake kwa KRG, Otile alisema kwamba anawasikia sana wabaya wake wakimzungumzia vibaya na anawaacha tu kwa sababu anajua hapo ndipo wanastahili kuwepo, kwenye mazungumzo yasiyo na tija.

“Nawasikia nyinyi wote mkizungumza matope nacheka tu kwa sababu hapo ndipo mnastahili kuwepo, watu wa mazungumza finyu na fikira mbaya. Mungu wangu ni wa makusudi, haendekezi ujinga ila anasamehe ajali,” Otile alimaliza.

Jana, KRG alimtuhumu kwamba licha ya kumsaidia, hajawahi hata siku moja kumsikia Otile akilitaja jina lake na kumshukuru kwa kumshika mkono Nairobi wakati hakuwa na kitu.