Zari afichua mpango wake katika ndoa na mumewe Shakib Cham ni kupata watoto 2

“Ndio lazima ni kweli tunatarajia kupata mtoto inshaallah, pengine wawili lakini kwanza tunatafuta mmoja," alisema.

Muhtasari

• Zari ni mama wa watoto 5, wawili wakiwa ni wale aliozaa na Diamond lakini kwa sasa wanalelewa na mume wake wa sasa, Shakib Cham.

Zari na Shakib
Zari na Shakib
Image: Screengrab, Instagram

Baada ya kufunga harusi ya Kiislamu ya Nikkah takribani mwaka mmoja uliopita, mwanasosholaiti Zari Hassan amefunguka kuhusu mipango na mustakabli wa ndoa yake na mumewe Shakib Lutaaya Cham.

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania wakati wa kuzindua chapa ya nepi ya Softcare, Zari alisema kwamba mpango wao ni kupata watoto wawili katika ndoa.

Zari alizipigia debe nepi hizo akisema kwamba atakuwa mmoja wa kina mama ambao watazitumia kwani anatarajia kupata mtoto na mumewe Shakib.

“Ndio lazima ni kweli tunatarajia kupata mtoto inshaallah, pengine wawili lakini kwanza tunatafuta mmoja, hiyo inamaanisha legacy ya nepi hizi itaendelea, namaanisha pia sisi tunatarajia kupata mtoto,” alisema.

Zari alisema kwamba chapa hiyo ya nepi imeenea katika mataifa takribani 15 na hivyo hawakukosea kumteua kama balozi wao wa mauzo kwani ana ushawizi katika mataifa mengi tu haswa ukanda wa Afrika Mashariki.

Zari ni mama wa watoto 5, wawili wakiwa ni wale aliozaa na Diamond lakini kwa sasa wanalelewa na mume wake wa sasa, Shakib Cham.

Alisema kwamba Shakib ni rafiki wake wa karibu na ndio maana anatembea naye kila mahali licha ya kwamba ubalozi huo Shakib si mwambata.

“Kila kitu kinawezekana lakini mimi ukiangalia vizuri mimi natembea na mume wangu. Yeye ni rafiki yangu, ni mwambata wangu katika ndoa, ananisapoti katika kila kitu changu, na hivyo ndivyo namtambua sana,” alisema.