Diamond amsifia Zuchu kwa kufikisha views milioni 100 kwa wimbo mmoja jukwaani YouTube

Diamond alisema kwamba Zuchu ameiheshimisha lebo yake kwani wimbo wa ‘Sukari’ ndio wa kwanza wa Kiswahili usio wa kolabo kufikisha views milioni 100 kutoka kwa msanii wa kike.

Muhtasari

• Kando na rekodi hiyo, Zuchu pia ni mionhoni mwa wasanii wa kike katika ukanda wa Sub Sahara mwenye wafuasi wengi Zaidi katika mtandao wa video wa YouTube.

Diamond amethibitsha kuachwa na Zuchu

Bosi wa lebo ya muziki ya Diamond Platnumz, WCB Wasafi amevunja kimya chake na kudhihirisha furaha baada ya msanii wake Zuchu kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha utazamaji wa milioni 100 kwenye wimbo mmoja.

Zuchu ambaye alisainiwa kwenye lebo hiyo mapema 2020 na wikendi iliyopita alifikisha views milioni 100 kwenye wimbo wake wa Sukari, ambao aliuachia miezi michache baada ya kusainiwa.

Kufuatia ufanisi huo, bosi wake ambaye pia anatajwa kuwa mpenzi wake hakuweza kuficha furaha yake na kumuonea fahari Zuchu akisema kwamba mrembo huyo wa Zanzibar ameipa heshima lebo ya WCB.

Diamond alisema kwamba Zuchu ameiheshimisha lebo yake kwani wimbo wa ‘Sukari’ ndio wa kwanza wa Kiswahili usio wa kolabo kufikisha views milioni 100 kutoka kwa msanii wa kike.

Ukiona kwa macho ni kama Jambo la kawaida, ila sasa unapojaribu kufanya ndio unajua uzito wake!! SUKARI By female artist 100% Swahili song! No feature! 100M viewers! Ni heshima kwa WCB wasafi, music industry na nchi," Diamond aliandika kupitia kwa insta story yake.

Kando na rekodi hiyo, Zuchu pia ni mionhoni mwa wasanii wa kike katika ukanda wa Sub Sahara mwenye wafuasi wengi Zaidi katika mtandao wa video wa YouTube.

Wimbo wa ‘Sukari’ umetajwa na wengi kuwa bora kuwahi kutoka kwa msanii Zuchu, ambaye baadhi wanahisi ameshindwa kuishi kwa matarajio ya wengi ambao wanasema vibao vingine ambavyo amekuwa akichilia havijawahi piku kiwango cha ‘Sukari’.