Zuchu afuta post zake zote za instagram

Mwimbaji wa Tanzania Zuchu ameweka kwenye kumbukumbu machapisho yake yote kwenye mitandao ya kijamii.

Muhtasari
  • Ukurasa wa instagram wa mwimbaji unasema "No post Yet" lakini una machapisho 26 yaliyohifadhiwa.
Zuchu
Zuchu
Image: Insta

Mwimbaji wa Tanzania Zuchu ameweka kwenye kumbukumbu machapisho yake yote kwenye mitandao ya kijamii.

Ukurasa wa instagram wa mwimbaji unasema "No post Yet" lakini una machapisho 26 yaliyohifadhiwa.

Kwenye instagram, watumiaji huweka machapisho kwenye kumbukumbu ili kuyarejesha ikihitajika.

Taarifa zinasema kuwa mwimbaji huyo anajaribu  kujitengenezea wakati wake katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ulioanza Jumatatu Machi 11 2024 na pengine utakamilika jumatano tarehe 10 Aprili 2024.

Ramadhani ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu na mwezi mtukufu wa mfungo ambao huanza na kumalizika kwa kuonekana kwa mwezi mpevu.

Wakati huo huo, Zuchu hivi karibuni aliomba radhi kwa Watanzania baada ya kufungiwa kutumbuiza Zanzibar.

Hayo yalijiri baada ya onyesho lake la Kendwa Rocks ambapo alitamka maneno ya matusi kwa mujibu wa Bosata ambalo ni Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania.

" Kutokana na sintaofahamu iliyojitokeza kwenye show yangu ya  Zanzibar, niombe radhi kwa jamii kama kuna sintofahamu yoyote iiliyojitokeza na kama kuna mtu yeyote ilimkers",aliomba msamaha.