Zuchu apigwa marufuku kutumbuiza Zanzibar baada ya kuimba matusi jukwaani

Awali tuliripo kuhusu barua ya Zuchu kwa baraza la Sanaa Tanzania, BASATA akiomba radhi kutokana na taharuki iliyozuka baada ya video yake akiimba matusi kutetea penzi lake kwa Diamond Zanzibar.

Muhtasari

• “Baraza hili lina wajibu wa kuangalia mienendo, maadili na tamaduni za Zanzibar,” alisema Omar Abdalla Adam, katibu wa baraza hilo.

Zuchu
Zuchu
Image: Insta

Varangati la Zuchu na mabaraza ya maadili nchini Tanzania linaendelea kuchukua mkondo tofauti na usiotarajiwa baada ya taarifa kudai kwamba msanii huyo amefungiwa kutumbuiza wala kufanya shoo yoyote katika kisiwa cha Zanzibar kwa miezi 6.

Kwa mujibu wa jarida la The Citizen, baraza la Sanaa kisiwani humo BASSFU kilibaini kwamba msanii huyo hakuwa amejiandikisha kwao kutumbuiza lakini pia adhabu hiyo imefuatia shoo ya Full Moon Party iliyofanyika usiku wa Februari 24 kisiwani humo.

 Kama tulivyoripoti awali, katika video iliyoonwa na radiojambo.co.ke, Zuchu akiwa jukwaani aliimba akiwasuta wanaotaka yeye na Diamond kuachana akisema kwamba msanii huyo kwake hatoki hata wampe mapenzi ya muingiliano kinyume cha maumbile.

Matamshi hayo yanayotajwa kuenda kinyume na maadili ya Wazanzibari wenye misimamo mikali ya kihafidhina yalisababisha BASSFU kuchukua hatua hiyo ya kumfungia mzawa wao.

“Baraza hili lina wajibu wa kuangalia mienendo, maadili na tamaduni za Zanzibar,” alisema Omar Abdalla Adam, katibu wa baraza hilo kama alivyonukuliwa na The Citizen.

“Kwa hiyo tumemfungia Zuchu kutojihusisha na shughuli yoyote ya kisanaa kisiwani Zanzibar kwa miezi 6 kuanzia leo hii,” aliongeza.

Kando na hapo, Zuchu alipigwa faini ya shilingi milioni moja kwa kutumbuiza Zanzibar bila kuwa na kibali chochote kwani walibaini kwamba yeye si mwanachana wa baraza hilo.

Awali tuliripo kuhusu barua ya Zuchu kwa baraza la Sanaa Tanzania, BASATA akiomba radhi kutokana na taharuki iliyozuka baada ya video yake akiimba matusi kutetea penzi lake kwa Diamond Zanzibar.