Jinsi Diamond alitumia wimbo wa Alikiba kumuomba msamaha Zuchu jukwaani (video)

Diamond akizungumzia video akitembea na Zari, aliimba akisema, "Fikira zako ziko vibaya, Na kudhani ya kwamba yule demu nilimpenda. Ni kweli nilimpenda. Lakini ni kama rafiki wa mtima."

Diaond na Zuchu kwenye ubora wao jukwaani.
Diaond na Zuchu kwenye ubora wao jukwaani.
Image: Screengrab//WasafiMedia

Wikendi iliyopita, Diamond walikutana na Zuchu kisiwani Zanzibar kwa ajili ya shoo ya pamoja – Full Moon Party.

Hii ilitokea muda mchache baada ya wawili hao, kila mmoja kubainisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba wameshaachana na kila mtu alikuwa anajishughulisha na hamsini za kwake kimaisha.

Lakini cha kushangaza ni kwamba Diamond alimua kufanya jambo lisilotarajiwa baada ya kupanda jukwaani pamoja na Zuchu na kuanza kumuimbia wimbo wa kimapenzi kama njia moja ya kumtaka radhi kwa nia ya kutaka warudiane kimapenzi tena.

Japo wengi wanaamini wawili hao wanafanya kufukuzia kiki kwa suala lao la kimapenzi, lakini kilichowashangaza wengi ni wimbo ambao Diamond aliutumia jukwaani kumuomba Zuchu msamaha.

Wimbo wa mpinzani wake, Alikiba – Mapenzi yana Run dunia.

Kwenye video, Diamond alionekana kupiga goti moja mbele ya Zuchu jukwaani huku umati ukishangilia na akaanza kuimba wimbo huo wa Alikiba akisema;

… Mwenzio mimi ni mtulivu, Na kuiba mali ya mtu sijafunzwa, Ona dhambi lawama. Ulonipa mimi leo inaniuma eh. Fikira zako ziko vibaya, Na kudhani ya kwamba yule demu nilimpenda. Ni kweli nilimpenda. Lakini ni kama rafiki wa mtima. Haya ulofanya leo, Ikifika kesho utajibu nini kiama. Kwa yale yote mapendo ni kama kioo, Aliyokupa niliyaona…”

Zuchu alikuwa wa kwanza kuthibitisha kuvunjika kwa penzi lao mwishoni mwa juma lililopita, jambo ambalo Diamond pia aliliafikia na kuwataka mashabiki wake kumuombea.

Zuchu alisema;

“Habari familia .ilibidi kupost hii ili kufuta dhamiri yangu. Kuanzia leo hii mimi na nasibu (diamond) hatuko pamoja,” Zuchu alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliongeza, “Najua hili limekuwa jambo letu lakini as hard as it is kumuacha mtu unaempenda hii naomba mungu iwe ya mwisho na nianze maisha mapya. Mapenzi ni heshima kwa bahati mbaya sana hiko kimekosekana kwetu.”

Diamond kwa upande wake aliandika;

“Basi bwana wadau, ndio kama Mlivyosikia Matikiti Yamenidondokea….hivyo nahitaji sana Maombi Yenu, Huruma na Ukaribu wenu kipindi hiki cha Ujane wangu, ili kupata nguvu na faraja kwenye Kipindi Hiki Kigumu😭😭😭.” 

Inaarifiwa Zuchu aliamua kumuacha Diamond baada ya kuona video yake wakitembea na babymama wake, Zari wakiwa wameshikana mikono.