Edday Nderitu atamka laana nzito kwa kina baba wanaokwepa jukumu la kulea watoto wao

Kwa mujibu wa Edday Nderitu, alitaka kina baba wa aina hiyo kutopana Amani katika nafsi zao, kwa kile alisema kwamba huwa wanawaacha watoto wadogo na maswali mengi ya kujibu.

Muhtasari

• Saroni ambaye ni mama wa watoto wa kiume anayeishi bila baba yao alimkabili mwanawe na moja ya swali zito kwa umri wake,.

Edday Nderitu.
Edday Nderitu.
Image: FACEBOOK// EDDAY NDERITU

Alhamisi, rafiki wa Edday Nderitu, Bernice Saroni alizua hisia mseto katika mtandao wa TikTok baada ya kurekodi video akiwa ndani ya gari na mmoja wa watoto wake wa kiume.

Saroni ambaye ni mama wa watoto wa kiume anayeishi bila baba yao alimkabili mwanawe na moja ya swali zito kwa umri wake, akitaka kujua hisia zake kuishi bila baba yake.

Swali hilo lilionekana kumtatiza mtoto huyo mdogo kiasi kwamba alijibu hajui kabla ya mamake kumbana Zaidi akimwambia kwamba anajua jinsi anahisi na angetaka kufahamu.

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake walimsuta kwa kumkabili mtoto mdogo na swali gumu hivyo huku wengine wakimhurumia mtoto huyo aliyeonekana kutatizika kiakili kutokana na swali hilo kutoka kwa mama yake.

Mmoja wa watu ambao walimhurumia mtoto huyo ni Edday Nderitu, mama wa watoto watatu ambaye anaishi na wanawe Marekani baada ya kuitoroka ndoa yake na mwanamuziki wa Mugithi, Samidoh.

Nderitu, ambaye pia amepitia changamoto si haba katika ndoa kabla ya kufanya uamuzi wa kuhama na wanawe kutoka nchini Kenya, alimsikitia mtoto wa Saroni na kwenda mbele kutamka laana nzito kwa kina baba wote wanaokepa majukumu wa kuwalea na kuwa karibu na wanao.

Kwa mujibu wa Edday Nderitu, alitaka kina baba wa aina hiyo kutopana Amani katika nafsi zao, kwa kile alisema kwamba huwa wanawaacha watoto wadogo na maswali mengi ya kujibu.

“Hii ni mbaya sana, hii ndio njia wanaume wanawafanya wanao kujihisi. Naomba kina baba wote wanaokwepa majukumu yao ya kulea watoto wao wasiwahi pata Amani katika nafsi zao,” Edday Nderitu alisema.