Nikita Kering alazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa na ngo'mbe aliyekuwa akimkamua

Ng’ombe alimtupia teke kabla ya kusambaratisha shughuli nzima na kutupa ndoo kando, huku Kering akionekana kupatwa japo kwa kiduchu na teke la ng’ombe na baadae kuonekana akiwa hospitalini na bendeji kwenye mguu wake wa kushoto.

Muhtasari

• Akinukuu video hiyo, Nikita Kering alisema kwamba ilikuwa kuonyesha matukio ya sikukuu ya pasaka kwa ujumla.

• Msururu wa video hiyo kwenye ukurasa wake ulionyesha matukio mengine ya jinsi sikukuu yake ya pasaka ilivyoanza.

NIKITA KERING
NIKITA KERING
Image: Instagram

Msanii Nikita Kering ameripotiwa kulazwa hospitalini baada ua kile kilichotajwa kama kujeruhiwa na ng’ombe aliyekuwa akimkamua shambani.

Katika klipu ambayo inaenezwa mitandaoni, msanii huyo mshindi wa tuzo alionekana akiwa amelazwa hospitalini baada ya awali kupakia klipu kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anamkamua ng’ombe shambani.

Katika video hiyo akiwa anakamua ng’ombe, Nikita alikuwa amevalia buti, jeans huku akiwa ameinaka kwenye maziwa ya ng’ombe akikamua huku akitabasamia kamera.

Akinukuu video hiyo, Nikita Kering alisema kwamba ilikuwa kuonyesha matukio ya sikukuu ya pasaka kwa ujumla.

Msururu wa video hiyo kwenye ukurasa wake ulionyesha matukio mengine ya jinsi sikukuu yake ya pasaka ilivyoanza, yakiwemo kuonekana jikoni akisonga ugali, akiandaa ‘mursik’ kabla ya tukio la kukamua ambalo lilimuendea mrama.

Ng’ombe alimtupia teke kabla ya kusambaratisha shughuli nzima na kutupa ndoo kando, huku Kering akionekana kupatwa japo kwa kiduchu na teke la ng’ombe na baadae kuonekana akiwa hospitalini na bendeji kwenye mguu wake wa kushoto.

Video hiyo ilipata hisia nyingi kutoka kwa watumiaji wa mtandao, wengine wakimuhurumia na wengine wakitaka kujua kwa nini alikuwa akikamua ng'ombe kwanza.

Tazama video hiyo jinsi sikukuu ya pasaka ilivyoanza vibaya kwa msanii huyo kutoka bonde la Ufa;