Diamond akanusha madai kwamba kofia aliyopokonywa na shabiki ilikuwa ya kichawi

Mwimbaji huyo aliongeza kuwa, yeye daima ni maalum na kwamba huwa hatumii uchawi na kofia yake ya kijani kibichi.

Muhtasari

• Mwimbaji huyo aliongeza kuwa, yeye daima ni maalum na kwamba huwa hatumii uchawi na kofia yake ya kijani kibichi.

Mkurugenzi mtendaji wa Wasafi Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz hatimaye amenyoosha maelezo yake kuhusu tukio la kuibiwa kofia akiwa miongoni mwa mashabiki na kuhaha kwelikweli kuifukuzia ile kofia ya rangi ya kijani.

Diamond ambaye alikuwa anazungumza na waandishi wa habari za burudani alasiri ya Alhamisi alitetea hatua yake ya kuhaha kuirejesha kofia hiyo akikanusha madai kwamba ilikuwa na hirizi zake.

Diamond alisema sababu iliyomfanya kuhangaika kuirudisha kofia ile ni kwa sababu ilikuwa ya kipekee ambayo aliipata kibahati.

Mwimbaji huyo aliongeza kuwa, yeye daima ni maalum na kwamba huwa hatumii uchawi na kofia yake ya kijani kibichi.

Kulingana na Platnumz, alihangaika kupata kofia hiyo alipotembelea Afrika Kusini akiwa hana kofia na alipokuwa katika harakati za kuipata, alihamia maduka tofauti hadi akapata kofia hiyo ya kipekee isiyokuwa na shimo nyuma.

Kofia nyingi alizokuwa akipata kulingana na Platnumz, hazikuwa za kipekee kama kofia ya kijani kibichi. Alidai katika baadhi ya maduka, aligongana na mengine mazuri, lakini aliweza kujua mengine ni madogo, mengine makubwa na machache hayawezi kukaa vizuri na kichwa chake.

“Na kiukweli watu wasiojua, hii kofia yangu sio ya kichawi.”

“Nikiwa South Africa, wakati mmoja nilihangaika sana kupata kofia kama hii na kitu kingine. Nilizunguka sana katika Malls karibu zote na nikapata hii moja tu. Na mara nyingi kichwa changu hupata taabu. Hupata nyingi kuwa ndogo na size yangu huwa special. Sasa nilipo bahatika kupata hii, nikafika Dodoma, nikaibiwa aaayi! Haiwezekani niache hivyo iende” alisimulia.

Baada ya mlinzi wake kumsaidia kupata kofia ya kijani kibichi, Platnumz aliongeza kuwa alikwenda Amerika na kununua kofia.

Diamond pia alizungumzia mahindani wake Alikiba kumiliki chombo cha habari na kusema kwamba katu hawezi kuona vibaya kwa hatua hiyo yake.

Diamond alimpongeza Alikiba kwa hatua hiyo na kutoa wito kwa wasanii wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo wazianzishe media ili kupanua wigo wa burudani lakini pia ajira kwa wengine.