“Sidondoki mpaka Mungu aseme imetosha!” Diamond kuhusu kuporomoka kimuziki

Hata hivyo, Diamond amesema kwamba hatima yake iko mikononi mwa Mungu na kamwe hawezi kudondoka na kuporomoka kwa maneno ya wanadamu hadi pale Mungu mwenyewe atakaposema imetosha.

Muhtasari

• Bosi huyo wa WCB Wasafi ambaye anasemwa kwamba miziki yake haijakuwa na kuchangamsha mashabiki kama ambavyo ilikuwa kipindi cha nyuma.

• Kando na kujizungumzia mweyewe, Diamond pia alifafanua kwa nini aliamua kuzika tofauti zake na Harmonize hivi majuzi.

Diamond na Harmonize
Diamond na Harmonize
Image: Hisani

Msanii Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amewajibu wanaomsema kwamba viwango vyake kimuziki vimedorora katika nyakati za hivi karibuni.

Bosi huyo wa WCB Wasafi ambaye anasemwa kwamba miziki yake haijakuwa na kuchangamsha mashabiki kama ambavyo ilikuwa kipindi cha nyuma.

Wengine wamekuwa wakimtaka kuchagua kutundika buti zake kimuziki angali bado juu kuliko kungoja hadi wasanii chipukizi kumdhalilisha kwenye Nyanja za muziki.

Hata hivyo, Diamond amesema kwamba hatima yake iko mikononi mwa Mungu na kamwe hawezi kudondoka na kuporomoka kwa maneno ya wanadamu hadi pale Mungu mwenyewe atakaposema imetosha.

Suala la kudondoka mimi sidondoki mpaka Mungu aseme. Yaani mimi nina mipango Zaidi na ngoma nyingi kali ambazo hazikatiki leo wala kesho mpaka mwenyezi Mungu akisema Diamond eeh sasa inatosha. Lakini kwa maneno ya watu mimi nina mawe, mimi nina nyimbo halafu muziki naujua sana,” Diamond alisema tena kwa kujishebedua.

Msanii huyo alikuwa akizungumza na waandishi wa habari za burudani mapema Alhamisi kuelekea tukio kubwa la tamasha la muziki litakalofanyika badae mwezi huu.

Kando na kujizungumzia mweyewe, Diamond pia alifafanua kwa nini aliamua kuzika tofauti zake na Harmonize hivi majuzi.

Wawili hao ambao wamekuwa wakihasimiana tangu 2019 walipataka kwenye hafla ya chakula cha futari na wakaonekana wakisalimiana kwa tabasamu.

Image: hisani,

Akizungumzia tukio hilo, Diamond alisema kwamba yeye anaishi vizuri na watu na kwamba haoni sababu ya kupanda mbegu ya chuki kwa watu aliowakuza kimuziki kama wanawe.

"Mimi naishi na watu vizuri sana, binadamu ana mapungufu yake kwa hiyo hawa wasanii wote Rayvanny, Harmonize wote mimi nawaitaga wanangu. Hata ilivyotoka chart ya Spotify niliandika Simba na wanawe, hata itokee kitu gani mimi moyoni mwangu hawa bado ni wanangu. Wanavyoenda kufanya vizuri huko nje sifa zinarudi kwangu... alilelewa na Diamond Platnumz."