Diamond atabiri wimbo wa 'Enjoy' kufikisha views 120M baada ya mwaka mmoja tangu kutolewa

Diamond akitabiri kuhusu ufanisi ujao Zaidi kwa video hiyo, alisema kwamba kama ndani ya miezi 7 video imefikisha views 70m, basi ndani ya miezi 10 itakuwa na views 100m na mwaka ukitimia itakuwa na views 120m.

Muhtasari

• Wasanii hao kupitia Instagram waliweka ufanisi huo ikionyesha kwamba video yao imevuka utazamaji wa milioni 70 ndani ya miezi 7 tu iliyopita.

Diamond na Jux
Diamond na Jux
Image: Instagram

Wasanii Diamond Platnumz na Juma Jux wanaendelea kusherehekea ufanisi mkubwa wa wimbo wao wa kolabo, Enjoy miezi 7 tangu kuachiliwa.

Wasanii hao kupitia Instagram waliweka ufanisi huo ikionyesha kwamba video yao imevuka utazamaji wa milioni 70 ndani ya miezi 7 tu iliyopita.

Diamond akitabiri kuhusu ufanisi ujao Zaidi kwa video hiyo, alisema kwamba kama ndani ya miezi 7 video imefikisha views 70m, basi ndani ya miezi 10 itakuwa na views 100m na mwaka ukitimia itakuwa na views 120m.

DUH 70Million kwa Miezi saba, God is Good!🏆…that means ikitimiza Miezi 10 itakua na 100M…na Mwaka itakua na 120M,” Diamond aliandika utabiri wake bila kuogopa.

Mwenzake Juma Jux alisisitiza kwamba huo ndio wimbo bora kwa mwaka wa 2023, akioneana kukinzana na kauli ambayo amekuwa akishikilia Harmonize kwamba wimbo wake wa Single Again ndio wimbo bora wa mwaka uliopita.

“70 millions 🙌🏾🙌🏾 nashukuru kwa upendo wenu! Bado mnaendelea kudhihirisha kwamba #enjoy i’ts a best song for 2023 east & central africa! 💪🏾 let’s hit 100 million before 1 year! Let’s Go!” Jux aliisisitiza.

Katika kipindi cha mwaka uliopita, nyimbo hizo mbili – Enjoy na Single Again – zimekuwa zikibishana kitakwimu katika majukwaa na program mbalimbali za kutiririsha miziki kidijitali.

Wasanii hao ambao pia ni washindani kimuziki wamekuwa wakitaniana, kila mmoja akivuta Kamba upande wake kwa kusifia wimbo wake kuwa bora.