Jux aachia kibao ‘Nisiulizwe’ baada ya kuachana na mpenziwe kabla ya siku ya Valentine’s

Jux na mpenziwe kabla ya kutengana, walikuwa wametangaza kwamba wapo karibu kumpata mtoto pamoja.

Muhtasari

• Jux baada ya maswali mengi mitandaoni ametangaza kuachia wimbo wake na title ya Nisiulizwe.

Jux na mpenziwe Karen Bujulu
Jux na mpenziwe Karen Bujulu
Image: Instagram

Mkali wa tungo za RnB kutoka Tanzania, Juma Jux ameachia kibao kipya ‘Nisiulizwe’ siku chache baada ya kudaiwa kuachana na mpenzi wake Karen Bujulu.

Kupitia ukurasa wake wa Instahram, Jux alitangaza Ijumaa alasiri kwamba kibao hicho tayari kimetoka na ujumbe mkubwa ndani mwake anataka kutoulizwa kitu chochote na mtu yeyote, haswa kuhusu penzi lake linalodaiwa kusambaratika.

Ujio wa kibao hicho unakuja siku chache baada ya kudaiwa kuachana na Karen Bujulu.

Siku ya wapendanao ya Valentino, Jux alionekana akisherehekea kwa maua na mama yake mzazi huku Karen Bujulu naye akionekana kuwa peke yake, licha ya wawili hao awali kuwadanganya watu kuwa walikuwa wanatarajia mtoto.

Jux na Bujulu wamekuwa katika uhusiano kwa kipindi cha kama miaka miwili hivi na wamekuwa wakiwapa matumaini mashabiki wao wa mitandaoni kuhusu kutarajia mtoto, jambo ambalo limekuja kubainika kuwa la uongo baada ya mimba kusubiriwa bila matumaini.

Siku ya wapendanao, Jux alimpa mama yake maua ndani ya gari lake na kusema kwamba ndiye mtu wa pekee ambaye anastahili mapenzi ya kweli na kila kitu siku ya wapendanao.

UPENDO WA HUYU MAMA NI NGUZO THABITI KATIKA MAISHA YANGU YA KILA SIKU! Jana ilikuwa siku nzuri sana kwetu. MY FOREVER VALENTINE to a special date – Because moms deserve all the love in the world. MOM! NAJUA UMEUMISS UWEPO BABA! As Long as mwanao nipo i’ll try my best kukupa furaha unayodeserve. HAPPY VALENTINES MOM🌹 NAKUPENDA SANA ️” Jux aliandika.

Karen na Jux awali walishafuta urafiki katika mtandao wa Instagram kwa kuacha kufuatana.