Vanessa Mdee afunguka kwa nini aliacha kutumia pombe miaka 4 iliyopita

Mdee alisema kwamba alipata watoto 2 ndani ya miaka 3 na kuwa sasa ni muda wa kutulia kuwalea watoto wake, akifichua kwamba tangu awe mzazi hajawahi enda mbali na nyumbani.

Muhtasari

•Katika mtoko huo wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mumew, ndio ilikuwa ziara ya kwanza tangu awe mama kuwa mbali na nyumbani kupunga upepo.

Vanessa Mdee
Vanessa Mdee
Image: Instagram

Msanii Vanessa Mdee amefichua sababu za kuacha matumizi ya vileo vya aina yoyote miaka minne iliyopita.

Mdee kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia msururu wa video kwenye instastories zake akiwa na mpenzi wake Rotimi ambaye alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Walikuwa kwenye boti baharini wakipunja maisha kwa kijiko kikubwa na Vanessa Mdee alifichua kwamba licha ya kujivinjari kwa kila kitu kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rotimi, lakini alisema kwaheri kwa matumizi ya vileo vyote miaka 4 iliyopita.

“Sijatumia kinywaji chochote cha kulewesha kwa karibia miaka 4, moja kati ya maamuzi bomba kabisa ambayo niliwahi kufanya, ahsante Mungu kwa neema,” Mdee aliandika.

Itakumbukwa mrembo huyo pindi tu baada ya kuweka mambo wazi kwamba yeye na Rotimi ni mtu na mpenzi wake, walipata watoto kwa ukaribu kabisa, watoto wote wawili wakipatikana ndani ya kipindi cha kama miaka mitatu hivi.

Kwenye chapisho jingine, Mdee alidokeza kwamba haikuwa rahisi kupata watoto wawili ndani ya miaka 3 na akasema kwamba sasa hivi ni muda wa kutulia kama mama wa familia akifuatilia makuzi ya watoto wake.

Katika mtoko huo wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mumew, ndio ilikuwa ziara ya kwanza tangu awe mama kuwa mbali na nyumbani kupunga upepo.

Katika moja ya video alizochapisha Instagram, Mdee na Rotimi walionekana kweney ufukwe wa bahari na akamuandikia ujumbe mtamu akisema kwamba yeye ni mzuri kwa kila kitu anachokifanya wakiwa pamoja si ucheshi tu bali pia hadi uzazi na urafiki.

“Kwa mtanashati zaidi, mkarimu zaidi, thabiti zaidi, wa kutia moyo zaidi, wa kweli zaidi, wa dhati kabisa, mwenye nguvu zaidi, wa kuchekesha zaidi kati ya Wanadamu wote ambao nimewahi kujua. Nimebarikiwa kukupenda. Happy Happy Happy Birthday Baby MUNGU MWENYEZI MUNGU akubariki. Hii ni moja ni maalum. Kila mtu tafadhali nisaidie kumtakia Mume wangu Furaha ya kuzaliwa🎈 Mdee aliandika.

Hivi majuzi, wawili hao kwa mara ya kwanza waliweka wazi nyuso za wanao wakati wakisherehekea sikukuu ya Thanks Giving nchini Marekani.