Rotimi na Vanessa Mdee waonesha sura za wanao katika video maridadi

Wanafamilia hao walitokea katika mtindo huo kuadhimisha siku kuu ya Thanksgiving ambayo hufanyika nchini Marekani kila Alhamisi ya nne ya mwezi Novemba.

Muhtasari

• Wapenzi hao walipakia video ya pamoja kwenye akaunti za Instagram wakiwa wamevalia mavazi ya waridi.

Rotimi na Vanessa Mdee.
Rotimi na Vanessa Mdee.
Image: Instagram

Taarifa zilizopo katika mitandao ya kijamii ni kumhusu mrembo wa Tanzania Vanessa Mdee na mpenzi wake kutoka Marekani mwenye usuli wa Nigeria, Rotimi baada yao kuonesha sura za wanao kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

Wapenzi hao walipakia video ya pamoja kwenye akaunti za Instagram wakiwa wamevalia mavazi ya waridi.

Wawili hao walionekana wakitembea kwenye video iliyohaririwa kuwaonesha wanakwenda aste aste na Rotimi alikuwa anamshika mkono kifungua mimba wao, Seven ambaye ni mtoto wa kiume huku Vanessa Mdee akiwa amebeba karibu na kifuani binti yao mdogo, Imani.

Walikuwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ambayo aghalabu hushuhudiwa katika kaya za Nigeria, huku mvulana wao kichwani akimalizia kwa kilemba maridadi.

Wanafamilia hao walitokea katika mtindo huo kuadhimisha siku kuu ya Thanksgiving ambayo hufanyika nchini Marekani kila Alhamisi ya nne ya mwezi Novemba.

Akiandika kwenye video hiyo ambayo imefutia watu Zaidi ya nusu milioni chini ya saa 12 tangu walipoichapisha, Rotimi alisema kwamba wanawe ndio zawadi kubwa Zaidi na zenye thamani isiyoweza kukadirika walipata kutoka kwa Mungu.

“Zawadi kubwa Zaidi ambazo tuliweza kubarikiwa nazo kutoka kwa Mungu,” waliandika.

Mashabiki kadhaa walimiminika kwenye upande wa koments na kuachia mapenzi yao kwa wanandoa hao wa nguvu ambao walibarikiwa na watoto wawili kwa mfululizo wa chini ya miaka 2.

“Wow, hii ni moto❤️❤️❤️Mungu bado namsubiri kwa subira Mfalme wangu ❤️❤️utaonekana mrembo 😍” Jelzthediva aliandika.

“Wanandoa wangu wa nguvu, nyie mnanifanya niamini katika mapenzi ya kweli, timu vanessa,” Yvonnechacks alisema.