Msanii DJ Gibbzy ashinda tuzo ya EAEA

Alikuwa akishindana na kuteuliwa na baadhi ya wasanii wakubwa katika kitengo hicho;

Muhtasari
  • Miongoni mwa waliohudhuria ni Dkt Ezekiel Mutua Mkurugenzi Mtendaji wa MCSK.
DJ GIBBZY

 Staa wa muziki kutoka Tanzania,produsa na rapa DJ Gibbzy ndio ameshinda tuzo ya Afrika Mashariki Tuzo za burudani za "Breakthrough Artiste of the year- Tanzania".

Alikuwa akishindana na kuteuliwa na baadhi ya wasanii wakubwa katika kitengo hicho;

Abigail Chams, DVoice, Mocco Genius na Bruce Africa.

Tamasha la  tuzo hizo ilifanyika Nairobi siku ya Jumapili usiku na kuhudhuriwa  na maafisa wa serikali mawaziri na baadhi ya wasanii.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Dkt Ezekiel Mutua Mkurugenzi Mtendaji wa MCSK.

Akiongea na wanahabari Gibbzy alisema;

“Hii ni hatua ya ajabu kwa kazi yangu, kwanza tuzo ya milele. Ninataka kuwashukuru mashabiki wangu kwa kunipigia kura na kunishikilia kila wakati kusambaza muziki wangu. Sitakuangusha kamwe. Muziki zaidi njiani