Notiflow atangaza kutafuta ‘bestie’ wa kiume, “marafiki wa kike walinigeuka na kuwa nyoka!”

Kwa muda mrefu, mpenzi huyo wa zamani wa Colonel Mustafa alikuwa na uhusiano wa karibu na mwanadada King Alami, katika uhusiano ambao ulikuwa na changamoto si haba.

Muhtasari

• “Marafiki zangu wote wa kike walinigeuka na kuwa nyoka, kwa hiyo ninataka kujaribu rafiki wa kiume safari hii,” Notiflow aliandika.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Notiflow

Natalia Flornce, rapa wa kike kutoka humu nchini maarufu kwa jina la kisanii Notiflow ametangaza kuwa anatafuta rafiki wa karibu wa kiume.

Kupitia insta story yake, Notiflow alitoa sababu akisema kwamba marafiki zake wote wa kike walimgeuka na kuwa nyoka.

Msanii huyo alisema kwamba yuko tayari safari hii kujaribu urafiki na wanaume.

“Marafiki zangu wote wa kike walinigeuka na kuwa nyoka, kwa hiyo ninataka kujaribu rafiki wa kiume safari hii,” Notiflow aliandika.

Kwa muda mrefu, mpenzi huyo wa zamani wa Colonel Mustafa alikuwa na uhusiano wa karibu na mwanadada King Alami, katika uhusiano ambao ulikuwa na changamoto si haba.

Wawili hao walikuwa wakiachana kisha kurudiana na kuachana mara kwa mara.

Mwaka jana, King Alami alisemekana kudondoka kutoka ghorofani na baadae familia yake ikaweza wazi kwamba alihitajika kukatwa mguu baada ya kile kilisemekana ni majeraha mabaya kutokana na kudondoka.

Familia ilieleza kuwa safari ya Alami ya kupona itakuwa ngumu lakini inatumai ataipitia kwani bado ni mchanga na ana mustakabali wake wote mbele yake.

Habari za kuanguka kwa Alami zilitangazwa na Notiflow, akisema kwamba alikuwa na huzuni zaidi.

"Moyo wangu umevunjika, na nimehuzunika, lakini ninaendelea kuwa chanya na kusali," aliandika.

Alieleza kuwa kuanguka kwake hakukuwa kwa bahati mbaya na kwamba suala hilo lingechukuliwa kama kesi ya jinai.