Noti Flow avunja kimya baada ya mpenziwe kudaiwa kujirusha kutoka kwa ghorofa

King Alami alidaiwa kuruka kutoka kwenye jumba alilokuwa hadi chini

Muhtasari

• Noti flow aliwaambia watu kuwa suala hilo ni la kutatuliwa na maafisa wa polisi ambao bado wanafanya uchunguzi wao.

•Alisema kuwa baada ya tukio hilo alizama kwenye hali ya huzuni na kudai alitumai kuwa ni ndoto.

Image: INSTAGRAM// NOTI FLOW

Rapi Notiflow amefunguka kuhusu saga ya aliyekuwa mpenzi wake King Alami aliyedaiwa kuruka kutoka kwenye nyumba ya ghorofa.

Kupitia Instagram, mwimbaji huyo alisema suala hilo ni la kibinafsi na halifai kuzungumziwa mtandaoni wala kutumika kuwashambulia.

Aliwaambia watu kuwa suala hilo ni la kutatuliwa na maafisa wa polisi ambao bado wanafanya uchunguzi wao.

"Naelewa kuwa nyote mnatutakia mema na mngetaka kujua kilichotendeka ila siwezi kuwaeleza. Haya ni mambo ya kihabusu yanayozingatiwa," alisema.

Alisema kuwa bado hajapata habari yoyote kuhusu kilichotendeka kwa kuwa hakuwa na King Alami siku hiyo.

Rapa huyo alisema Alami hana majeraha yoyote na kueleza  matumaini yake kuwa mpenzi huyo wake wa zamani atakuwa sawa.

"Ninachojali sana ni kuwa King Alami atapona na kutoka hospitalini. Kama kunaye aliyesababisha hiki natumai kitakurudia. Nawashukuru nyote kwa maombi yenu ," rapa huyo alisema.

Alisema kuwa baada ya tukio hilo alizama kwenye hali ya huzuni na kudai alitumai kuwa ni ndoto.

King Alami alidaiwa kuruka kutoka kwenye jumba hilo baada ya kuwa na mabishano na anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa hivi sasa.

Familia yake iliwaomba wanamitando msaada wa kifedha ili waweze kugharamia matibabu ya hospitali ambapo amelazwa.

Noti Flow pia alisaidia familia ya King Alami kuomba msaada.

Noti Flow na King Alami ambao wote ni wasagaji walikuwa kwenye mahusiano kwa takriban mwaka mmoja kabla ya kutengana.