“Kuzama katika penzi lako ilikuwa nje ya uwezo wangu!” – Musila amwambia Guardian Angel

“Kukutana na wewe ilikuwa hatima. Kuwa mke wako lilikuwa chaguo. Lakini kukupenda ilikuwa nje ya uwezo wangu. Asante kwa kuwa mwenzi mzuri wa maisha,” Esther Musila alimwandikia Guardian Angel.

Muhtasari

• Kupitia Instagram, Musila alichapisha video wakitembea kwa madaha na mumewe huku wakicheka kwa furaha.

• Katika video hiyo, aliambatanisha ujumbe jinsi alijipata kumpenda Guardian Angel licha ya utofauti mkubwa baina ya umri wao.

Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Esther Musila na mumewe Guardian Angel
Image: YouTube

Esther Musila ameendelea kuthibitisha mapenzi yake kwa mumewe Guardian Angel kwa kumkumbusha kila muda jinsi alivyombadilisha baada ya kumpenda bila vikwanzo licha ya pingamizi nyingi kutoka kwa baadhi ya watu.

Kupitia Instagram, Musila alichapisha video wakitembea kwa madaha na mumewe huku wakicheka kwa furaha.

Katika video hiyo, aliambatanisha ujumbe jinsi alijipata kumpenda Guardian Angel licha ya utofauti mkubwa baina ya umri wao.

Musila alisema kwamba yeye kukutana na Guardian Angel ilikuwa ni hatima iliyopangwa na Mungu lakini kukubali kuwa mke wake ulikuwa ni uamuzi wake pasi na kushurutishwa.

Mama huyo wa watoto watatu alithibitisha kwamba jinsi alijipata amezama katika penzi la kijana huyo wa muziki wa injili ni jambo ambalo hata yeye haelewi kwani lilikuwa nje ya uwezo wake kulizuia, huku akimsifia na kumshukuru kwa kuwa mwenzi wa kupigiwa mfano katika kipindi cha Zaidi ya miaka miwili tangu kufunga ndoa.

“Kukutana na wewe ilikuwa hatima. Kuwa mke wako lilikuwa chaguo. Lakini kukupenda ilikuwa nje ya uwezo wangu. Asante kwa kuwa mwenzi mzuri wa maisha,” Esther Musila alimwandikia Guardian Angel.

Mwezi mmoja uliopita, Musila katika moja ya podikast yake kwenye YouTube alifunguka jinsi Guardian Angel amembadilishia mtazamo wake wa mapenzi na kuwa mke kwenye ndoa.

Kwa maneno yake, Musila alikiri kwamba hakuwahi kufurahia ndoa yake ya kwanza kama ambavyo anafurahia ndoa yake na Guardian Angel.

Musila alisema kwamba pengine hilo ni kutokana na kwamba aliingia kwa ndoa akiwa mdogo sana kiumri, jambo ambalo lilimfanya kutopata furaha kwenye ndoa, akisema kwamba kwa sasa ana furaha ya kuitwa mke wa mtu.