“Mume wangu namlisha ugali na kuku” Mkewe Savara mwenye asili ya Japani akizungumza Kiswahili

“Sasa wengine eti wanataka bibi yangu aongee, sasa ndiye huyu, mama Chimmy” Na kumtaka kusema neno kabla ya Endo kuanza, “Habari zenu, huyu ni mume wangu huwa namlisha poa ugali na kuku.”

Muhtasari

• Wawili hao ambao hivi majuzi waliweka hadharani uhusiano wao, wanaaminika walianza kuchumbiana mwaka wa 2018 lakini mwanzoni, walichagua kuuficha.

 

Savara na mkewe Endo.
Savara na mkewe Endo.
Image: screengrab

Yvonne Endo, mkewe msanii wa kundi la muziki lililosambaratika la Sauti Sol amewafurahisha wengi katika mtandao wa Instagram na TikTok baada ya kurekodiwa akizungumza Kiswahili kumsifia mumewe.

Endo, ambaye ni mkaazi wa humu nchini mwenye asili ya Japani katika video hiyo walikuwa wamekumbatina na mumewe Savara huku akimtambulisha kwamba watu walimtaka azungumze.

Savara alimtambulisha kama mama Chimmy akisema, “Sasa wengine eti wanataka bibi yangu aongee, sasa ndiye huyu, mama Chimmy” Na kumtaka kusema neno kabla ya Endo kuanza, “Habari zenu, huyu ni mume wangu huwa namlisha poa ugali na kuku.”

Wawili hao walikutana kweney tamasha moja jijini Nairobi miaka michache iliyopita na Endo alisema kwamba mara ya kwanza Savara kujitambulisha kwake, alisema yeye alikuwa mtu wa kufanya kazi katika kumbi za starehe jijini.

“Kwa hiyo, nilikutana na Savara kwenye tamasha la African Nouveous, nilikuwa nimeenda pale na dada yangu. Ilikuwa karibu wakati wangu kuondoka alipojitambulisha…Alitaja kuwa yeye ni mtumbuizaji wa kuvua nguo na nikasema, “Sawa hiyo inachekesha sana”… Kisha mwisho wa usiku akaomba namba yangu,” alisema katika mahojiano ya awali

Wawili hao ambao hivi majuzi waliweka hadharani uhusiano wao, wanaaminika walianza kuchumbiana mwaka wa 2018 lakini mwanzoni, walichagua kuuficha.

Hata hivyo, katika mahojiano mengine, Savara alifichua kwaba hana mpango wa kumvisha pete mpenzi huyo akisema kuwa pete haina maana yoyote kwa vile tayari katika moyo wake wa mapenzi, ameshamvisha pete Endo.

"Pete ni ishara tu ya kitu. Wapo walio na pete huku nje, na hawafurahii. Kwangu mimi, nilichonacho na Yvonne ni kikubwa kuliko pete. Ingawa ni ishara ya kujitolea, sitakubali shinikizo. Tayari nimeweka pete moyoni mwangu. Siwasikilizi wanaochukia kwani ninatatua matatizo yangu peke yangu. Na mimi huweka mzunguko wangu mdogo sana,” alisema.

Mpenzi wa Savara Yvonne Endo ni mjasiriamali mwenye asili ya Japani anayeishi Kenya ambaye alikulia Nairobi na anaendesha mstari wa mavazi ya kifahari na dadake, Patti Endo.