Femi One atangaza kuuza baadhi y nguo zake ambazo hatumii, “zingine nilivaa tu mara moja!”

“Kwa hiyo, kama baadhi yenu mtakuwa na hamu ya kuzinunua, na zingine pia nitakuwa napatiana bure, hebu nijulishe kama hili ni jambo ambalo nyinyi watu mtakuwa mnalikubali," Femi alisema.

Muhtasari

• Rapa huyo alisema kwamba aligundua kuna baadhi ya nguo zake kwenye kabati la nguo ambazo alivaa tu mara moja na kuzisahau, zingine akisema zimeshakuwa ndogo kwa mwili wake.

FEMI ONE
FEMI ONE
Image: instagram

Rapa machachari wa kike kutoka humu nchini, Femi One ametangaza mpango wa kuziweka sokoni baadhi ya nguo zake ambazo kwa muda mrefu amegundua hajawahi kuzitumia.

Kupitia klipu fupi ambayp alipakia kwenye insta stories zake, Femi One alisema kwamba anaomba maoni kutoka kwa mashabiki wake jinsi ya kuanza shughuli hiyo ya kuziuza.

Rapa huyo alisema kwamba aligundua kuna baadhi ya nguo zake kwenye kabati la nguo ambazo alivaa tu mara moja na kuzisahau, zingine akisema zimeshakuwa ndogo kwa mwili wake.

Mrembo huyo alifichua kwamba ametathmini mpango wa kupeana zingine bure kama zawadi na zingine kuziweka okoni, akiwaomba mashabiki wake kumchorea mpango madhubuti wa jinsi ya kufanya hivyo, ikiwezekana pia kufungua akaunti mpya kwa ajili ya biashara hiyo ya haraka.

“Habari zenu watu wangu, nimegundua tu kwamba niko na mavazi mengi sana, mengine ambayo nimevaa kwa mara moja tu, mengine yamekuwa madogo, mengine nimetumbuiza kwenye matamasha nayo lakini sijawahi yavaa tena,” Femi One alianza.

“Kwa hiyo, kama baadhi yenu mtakuwa na hamu ya kuzinunua, na zingine pia nitakuwa napatiana bure, hebu nijulishe kama hili ni jambo ambalo nyinyi watu mtakuwa mnalikubali, au pengine kama ni kufungua ukurasa mwingine mahususi kwa biashara hiyo, hebu nipatieni mapendekezo yenu ya jina la utambulisho,” aliomba.

Tazama video hiyo hapa;